ARSENAL iliyo chini ya kaimu kocha Freddie Ljungberg ikiwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Emirates ilishindwa kufurukuta mbele ya Brighton kwa kuchapwa mabao 2-1 na kuchana mikeka ya watu.


jambo lililomkasirisha bosi aliyeshudia bao moja pekee likifungwa na Alexander Lacazzette dakika ya 50 huku mawili ya mpinzani wake aliyashuhudia dakika ya 36 likifungwa na Adam Webster na la ushindi lilifungwa na Neal Maupay dakika 80.

Ljungberg amesema kuwa wachezaji wake walicheza chini ya kiwango hali iliyofanya washindwe kupata ushindi kwenye mchezo huo.


Matokeo hayo yanaifanya Arsenal iwe nafasi ya 10 baada ya kucheza jumla ya mechi 15 na ina pointi 19 tu kibindoni huku Brighton wakiwa nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 15 ina pointi 18.

Arsenal imeshindwa kupata ushindi kwenye mechi zake mbili za mwezi Desemba ambazo zinasimamiwa na Kocha wa muda Ljungberg aliyepokea mikoba ya Unai Emery aliyedumu klabuni hapo kwa muda wa miezi 18.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.