RASMI sasa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amepigwa chini ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na kile kilichoelezwa kimetokana na matokeo mabovu ya msimu huu ndani ya Ligi na mechi za Kimataifa.

Habari zimeelezwa kuwa leo Yanga imeachana na Zahera ambaye msimu uliopita aliongoza Yanga kucheza mechi 18 za Ligi Kuu Bara bila kufungwa mpaka ilipodondokea pua mbele ya Stand United uwanja wa Kambarage kwa kufungwa bao 1-0.

Nafasi yake kwa sasa inachukuliwa na Kocha wa zamani wa timu ya Taifa, Charlse Boniface Mkwasa (Mkwasa Master) atakayekaimu kwa muda wa wiki mbili kabla ya kumpata Kocha Mkuu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.