UWANJA wa Nangandwa Sijaona leo mkoani Mtwara, Ndanda FC itaikaribisha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuwa na ushindani wa kipekee kwa timu zote Ila rekodi za mabao zinaibeba Yanga mbele ya Ndanda.
Ndanda
FC tangu ipande daraja msimu wa 2014 haijawahi kuifunga Yanga mabao
zaidi ya mawili na katika mechi 10 ambazo wamekutana Yanga imeshinda
mechi nne tofauti na Ndanda ambao wameshinda mechi moja pekee na
kulazimisha sare tano.
Pia
Ndanda imeifunga Yanga jumla ya mabao sita pekee huku Yanga ikiifunga
Ndanda mabao 12 kwenye jumla ya mabao 18 ambayo yamepatikana.
Mchezo mmoja tu wa msimu wa 2016-17 ulileta mabao mengi ambapo Yanga ilishinda jumla ya mabao 4-0 Uwanja wa Taifa.
Rekodi
za Uwanja wa Nangandwa zinaonyesha kuwa Yanga imefunga mabao mengi
kuliko Ndanda kwani kwenye mechi nne ambazo wamekutana Yanga imefunga
mabao matatu huku Ndanda ikifunga mabao mawili pekee na kwenye kushinda
Yanga imeshinda mara moja na imepoteza mara moja huku ikilazimisha sare
mechi mbili.
Mechi
moja ya msimu wa 2015/16 haikuchezwa Nangwanda kutokana na makubaliano
maalumu ilichezwa Taifa na timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana
mabao 2-2.
Post a Comment