IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa timu ya Azam FC amesema kuwa hesabu za kupata pointi tatu leo mbele ya Biashara United zipo miguuni mwa wachezaji wakiongozwa na safu ya ushambuliaji iliyo chini ya Obrey Chirwa na Donald Ngoma.
Azam
FC leo itamenyana na Biashara United uwanja wa Azam Complex ikiwa na
kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar
uliochezwa uwanjani hapo wikiendi iliyopita.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa tatizo kubwa lipo kwenye suala la
umaliziaji nafasi wanazozitengeneza jambo lililowafanya watumie muda
mwingi kuwapa makali washambuliaji wake.
"Tatizo
ndilo ambalo tunalifanyia kazi siku zote kwenye nafasi ya ushambuliaji,
jambo la kwanza tumekuwa tukicheza mechi za kirafiki kuwaongezea
kujiamini na kuongeza ukaribu kwa washambuliaji ikiwa ni pamoja na Ngoma
pamoja na Chirwa.
"Imani
yetu ni kuona tunapata matokeo mbele ya Biashara United ndio maana
tumewapa kazi kubwa washambuliaji na tunahitaji pointi tatu muhimu
mashabiki watupe sapoti," amesema Cheche.
Mchezo
wa Leo utakuwa wa tatu kwa Kocha Mkuu Arstica Cioaba raia wa Romania
kukaa kwenye benchi alionja joto ya kupoteza kwa Ruvu Shooting kwa
kufungwa bao 1-0 na sare mbele ya Kagera Sugar.
Post a Comment