MANCHESTER United imemnyoosha kocha wao wa zamani Jose Mourinho ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Spurs kwa kumtandika mabao 2-1.
Mchezo huu wa Ligi Kuu England umechezwa uwanja wa Old Trafford ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu Mourinho apigwe chini ndani ya Manchester United iliyo chini ya Ole Gunnar Solsjkaer kwa sasa.
Mshambuliaji tegemeo wa Manchester United, Marcus Rashford alifungua akaunti ya mabao kwa United dakika ya sita akifunga bao kali kabla ya Delle Alli wa Spurs kusawazisha dakika ya 39.
Bao hilo la Alli kidogo VAR ilikatae kutokana na hisia kwamba aligusa mpira kwa mkono mwisho timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili dakika ya 48, Rashford alichezewa rafu ndani ya 18 na mwamuzi kuamua ipigwe penalti ikazimishwa kimiani na Rashford mwenyewe dakika ya 49.
Post a Comment