TIMU ya Chelsesea iliyo chini ya Frank Lampard imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya  Aston Villa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliohezwa uwanja wa Stamford Bridge.

Tammy Abraham wa Chelsea alifunga bao la kwanza dakika ya 24 likasawazishwa na Mahamoud Hassan dakika ya 41 na kupelekea timu zote kwenda mapumziko zikiwa na sare ya kufungana bao 1-1.

Kipindi cha pili Chlesea iliongeza nguvu kwenye mashambulizi na ilipata bao la ushindi dakika ya 48 kupitia kwa Mason Mount.

Mshambuliaji Tammy Abrah hakuwa na bahati kwani alikosa nafasi nyingi za wazi ambazo zigeisaidia timu yake kushinda mabao mengi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.