Nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amezidi kujiweka sokoni baada ya kufi kisha wastani wa mabao matatu aliyofunga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo mwenye ndoto ya kuchezea Ligi Kuu England msimu ujao, juzi aliifungia timu yake ya KRC Genk bao dakika 85 licha ya timu yake kupoteza kwa mabao 4-1 Salzburg ya Austria katika nchezo wa Kundi E uliopigwa kwenye Uwanja wa Luminus Arena Genk.
Samatta alifunga mabao mengine kwenye kundi hilo walipokutana wawili hao ingawa walifungwa tena mabao 6-2 Septemba 17 katika kwenye Uwanja wa Red Bull Arena yeye ndiye alipachika bao la pili kwa upande wa timu yake.
Bao lingine Samatta alifunga dhidi ya mabingwa wa tetezi wa taji hilo, Liverpool Novemba 5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Anfield.
Hata hivyo, Napoli itamenyana na Genk katika mchezo wa mwisho wa kundi Desemba 10 kwenye Uwanja wa San Paolo, huku ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa na Mtanzania huyo katika kundi hilo.
Takwimu hizo zinaonekana kumbeba nyota huyo wa Kitanzania ambaye kimsingi kasi na uwezo wake umekuwa funzo kwa wachezaji wengi wanaochipukia kwenye mchezo huo
Post a Comment