Baada ya kutangaza kutundika daruga katika timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', beki wa Simba, Shomari Kapombe, amewapongeza Azam FC kwa msaada waliompatia wakati anaichezea timu hiyo.

Kapombe amefunguka kupitia kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM akisema hakika walikuwa na msaada mkubwa kwake maana alipitia kipindi kigumu akiwa anaumwa.

Alieleza kuwa wakati anatua Azam alipatwa na tatizo la damu kuganda kwenye kifua chake lakini Azam walimsaidia kupata matibabu mpaka akapona na akarejea kazini.

Ameeleza licha ya kuwa ameshaondoka na sasa yupo Simba hataweza kuwasahau kwa mchango wao waliompa kipindi hicho na akiwamwagia pongezi.

"Kwakweli nawashukuru sana Azam FC licha ya kuwa sipo nao kwa sasa, walinisaidia kipindi hali yangu ikiwa mbaya kabla sijarejea Simba.

"Walijitoa kunisaidia mpaka nikapata matibabu na nikawa nimepona, daima nitawakumbuka.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.