MAKUNDI ya michuano ya Kombe la Euro yalipangwa juzi huku kukiwa na kundi la kifo ambalo lilizua gumzo. Michuano ya Euro itafanyika mwakani ikiwa inasubiriwa na mashabiki wengi sana duniani kote.
Kundi F, ambalo limepangwa timu za Ujerumani, Ufaransa na Ureno huku likisubiri mshindi mmoja katika playoff, limekuwa gumzo sana kwenye mitandao na kwenye magazeti kadhaa makubwa duniani kote.
Hata hivyo, gumzo lingine ni kwamba kwenye hatua ya 16 Bora, England watakutana na moja kati ya timu itakayovuka hapo.
Pamoja na kwamba England wameshindwa kupangwa kwenye kundi hili, lakini bado hawapo salama sana kwa kuwa watakutana na moja ya timu hizo kwenye hatua ya 16 Bora kama watafuzu.
England wamepangwa kwenye Kundi D, ambalo kwa jinsi ratiba hii ilivyopangwa washindi wa hapa ndiyo wanakutana na kundi hilo la kifo.
Kundi A ni Uturuki, Italia, Wales na Uswisi, Kundi B ni Denmark, Finland, Ubelgiji na Urusi.
Kundi C, Uholanzi, Ukraine, Austria na mshindi kutoka playoff.
Kundi D; England, Croatia, Czech na wa kutoka playoff.
Kundi E; Hispania, Sweden, Poland na wa playoff.
Kundi F; Ureno, Ufaransa, Ujerumani na wa playoff.
Post a Comment