ZINEDINE Zidane amekataa kurudi nyuma katika vita yake ya maneno na Klabu ya PSG kuhusiana na sakata la Kylian Mbappe.
Kocha huyo wa Real Madrid hivi karibuni alitamka wazi kuwa Mfaransa mwenzake huyo ana ndoto ya siku moja kuichezea Real, kauli ambayo imewavuruga vigogo wa PSG wakiongozwa na Mkurugenzi wa Masuala la Michezo, Leonardo.
Kigogo huyo amemtaka Zidane aache kumchanganya Mbappe lakini bosi huyo wa Real Madrid ameshikilia msimamo wake.
“Yote niliyosema ni mambo ambayo Mbappe ameshayatamka mwenyewe kwamba ilikuwa ni ndoto yake siku moja kuvaa jezi nyeupe za Real Madrid,” alisema Zidane.
“Hicho ndicho nilichokisema na ninasema tena leo na nitarudia kila siku. Sina cha kusema zaidi kuhusu Leonardo, naweza kusema chochote ninachotaka.”
Leonardo awali alisema: “Kweli inaudhi, siyo mara ya kwanza hili limetokea. Nadhani kwamba sasa siyo muda wa kuzungumza kuhusu hili. Ni mchezaji ambaye amebakiza miaka miwili na nusu katika mkataba nasi, kwa hiyo kuzungumza kuhusu ndoto zake kila mara tukiweka pozi itakuwa ni vyema
Post a Comment