Manchester United wanapanga mikakati ya uhamisho msimu ujao ili kuweza kusaini mkataba na mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26, kwa mara ya pili na wako tayari kulipa pauni milioni 70 kwa ajili ya kijana huyo raia wa Ivory Coast, ambaye alikuwa nao baina ya mwaka 2013 na 2015. (Sun)
Unaweza pia kusoma:
- Watu 120 wakiwemo wapenzi wa jinsia moja wakamatwa Uganda
- Tanzania: Waziri Jafo akana kauli yake kuhusu wagombea
- Polisi wa Rwanda wawaua watu wawili mpakani
Liverpool wako katika mazungumzo ya mwisho kusaini mkataba na winga Mskotishi Ryan Fraser, mwenye umri wa miaka 25, utoka Bournemouth mwezi Januari. (Talksport)
Tottenham wako tayari kuweka dau la pauni milioni 50 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Lyon Nemphis Depay mwenye umri wa miaka 25 ambaye aliichezea Manchester United kati ya mwaka 2015 na 2017. (Mirror)
Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso, mwenye umri wa miaka 37, na meneja wa sasa wa Tottenham manager Mauricio Pochettino, mwenye umri wa miaka 47, wako katika orodha ya watu wanaoweza kuwa meneja wa Bayern Munich ajae(Star)
Manchester United haitajaribu kusaini mkataba na mshambuliaji wao wa zamani Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 38, katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari. Ibrahimovic yuko huru kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake na LA Galaxy utakapomalizika. (Sky Sports)
Mlindalango wa Arsenal Mjerumani Bernd Leno, ambaye sasa ana umri wa miaka 27, anaangaliwa na Bayern Munich kama changuo lao nambari moja na kuchua nafasi ya Manuel Neuer ambaye sasa ana umri wa miaka 33. (sun)
Borussia Dortmund bado wanamtaka mchezaji wa safu ya mashambulizi ya kati Anthony Gordon,mwenye umri wa miaka 18, licha ya dau lao la msimu uliopita la kumchukua mchezaji huyo wa timu ya kimataifa ya England ya vijana wenye chini ya umri wa miaka 19 kukataliwa.(Football Insider)
Wolves wamefikia kiwango cha juu cha mazungumzo ili kuweza kusaini mkataba na kiungo wa kati Chem Campbell mwenye umri wa miaka 16 kutoka Wales ,licha ya klabu za Ujerumani Borussia Dortmund, Schalke na RB Leipzig kuonyesha nia ya kutaka kumchukua. (Football Insider)
Meneja wa Arsenal Unai Emery atapewa michezo sita kuthibitisha ikiwa bado ni mtu anayefaa kwa kazi hiyo katika uwanja wa Emirates.(Standard)
Meneja wa zamani wa Uhispania boss Luis Enrique, ambaye amekuwa akitajwa kuwa ndiye mtu mwenye umwezekano wa kuchukua nafasi ya Emery katika Gunners, hana haja ya kurejea katika nafasi hiyo ya utawala kwa sasa . (ESPN)
Kiungo wa kati wa Newcastle Matty Longstaff, mwenye umri wa miaka 19, atasaini mkataba mpya katika kipindi cha wiki chache zijazo , lakini kaka yake mwenye umri wa miaka will sign a new contract in the next few weeks but hise zijazo , lakini kaka yake mwenye umri wa miaka 22 Sean ameambiwa kuwa atahitaji kutia bidii zaidi katika kipindi cha miezi ijayo 12 ili apate mkataba mpya . (Telegraph)
Mshambuliaji wa safu ya kati wa Uhispania Ayoze Perez, mwenye umri wa miaka 26, amefichua kuwa alikataa kuhamia has Valencia ili ajiunge na Leicester kutoka Newcastle msimu ujao. (Mail)
Tottenham, Chelsea, Watford na Norwich wako tayari kuweka dau kwa ajili ya kumpata mshambuliaji wa klabu ya Metz Habib Diallo Mwezi Januari . Msenegali huyo mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao manane katika michezo 13 katika msimu huu hadi sasa . (Teamtalk)
West Ham wanaangalia uwezekano wa kumnunua mlindalango mpya mwezi Januari baada ya kuongezeka kwa hofu juu ya hali ya kimchezo ya Roberto. Roberto mwenye umri wa miaka 33 kutoka Uhispania amekwishafungwa mabao 13 katika michezo sita ya Primia Ligi tangu alipojiunga na klabu hiyo baada ya kujeruhiwa kwa Lukasz Fabianski. (The Athletic - subscription required)
Inter Milan wana nia ya kumchukua kiungo wa mashambulizi wa Ubelgiji Dries Mertens, mwenye umri wa miaka 32, ambaye mkataba wake na Napoli unafikia ukingoni msimu ujao.
Klabu San Siro pia iko makini na mchezaji wa Paris St-Germain mwenye umri 28- -Thomas Meunier wa Ubelgiji na mchezaji mwenzake katika safu ya ulinzi Layvin Kurzawa, mwenye umri wa miaka 27, wa Ufaransa. (Calciomercato)
Post a Comment