Stars iliyo chini ya Etienne Ndayiragije ilianza kwa kasi kipindi cha kwanza haikuweza kutumia vema nafasi saba za kipindi cha kwanza na kuruhusu wapinzani wao Equatorial Guinea kuandika bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Pedro Obiang liliwapeleka Stars mapumziko wakiwa nyuma kwa mbao huo uliofungwa nje ya 18.
Kipindi cha pili Stars ilianza kwa kulazimisha mashambulizi na iliwapeleka mpaka dakika ya 68 ambapo Simon Msuva aliandika bao la kwanza akimalizia pasi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala' na kuweka mzani sawa.
Salum Abubakari alimaliza ile fujo isiyoumiza dakika 90 kwa kulipa mbao wa Obiang akiwa nje ya 18 kwa kuachia mshuti wake wenye uzito uliomshinda mlinda mlango wa Equatorial Guinea akimalizia pasi ya Ditram Nchimbi.
Ushindi huo unaifanya Stars kujikusanyia pointi zake tatu leo ikiwa kwenye uwanja wa Taifa
Post a Comment