Tunaweza kusema historia imeandikwa na klabu ya Simba kwa kufanikiwa kuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unaelekea kukamilika siku za usoni.
Simba ilianza kujenga uwanja huo miaka kadhaa iliyopita wakati wa utawala wa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage lakini haukwenda kwa kasi kutokana na uchumi kuwa mbaya.
Uwanja huo ambao upo Bunju jijini Dar es Salaam uhusisha viwanja viwili ambapo mmoja ni wa nyasi asili na mwingine wa bandia ambavyo vyote vitatumika kwa ajili ya mazoezi.
Simba watatumia uwanja wa nyasi asili kwa ajili ya mechi ambazo watakuwa wanachezea kwenye viwanja vya mikoani na halikadhalika bandia endapo wakipangiwa kukipiga Uhuru Stadium ama Taifa, Dar es Salaam.
Ni zaidi ya miaka 80 Simba wamekuwa hawana uwanja wa mazoezi sawa na Yanga ambao nao wameanza mchakato wa kuanza kujenga.
Taarifa zilizopo ni kuwa Simba wanaweza kuanza kutumia uwanja wa Bunju mapema mwezi ujao na watakuwa wanaandika historia ya kuwa timu ya kwanza dhidi ya watani zao wa jadi Yanga kumiliki kiwanja hicho.
Post a Comment