Kuelekea dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema atatoa tathimini ya wachezaji wapya anaowahitaji ikiwa ni pamoja na wakukatwa ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo mapema wiki ijayo. Imeelezwa.

Taarifa imesema kuwa Mkwasa ameshaanza kuufanyia kazi mchakato huo na atatoa tathimini ya wachezaji wanaopaswa kuongezwa na kuachwa kwenye kikosi hicho kwa ajili ya kuanza mchakato mpya wa kusajili wachezaji atakaowahitaji.

Mkwasa alisema baada ya kukutana na Kamati ya Ufundi, watashauriana na kufanya uamuzi wa
pamoja kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho wa kikosi wanachokihitaji kuendelea nacho katika vita ya
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya Kombe la FA nchini.

"Kwa muda ambao nimekaa na timu, tayari nimeshaanza kuifanyia kazi ripoti ya kiufundi, hadi wiki
ijayo nitakuwa nimekamilisha ripoti yangu ya kiufundi kuhusu usajili wa dirisha dogo, ila
nitawasiliana na Kamati ya Ufundi kwa ajili ya ushauri zaidi," alisema Mkwasa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.