MASOUD Djuma aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba na kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2017-18 akiwa na Mfarasa Pierre Lechantre inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu ya KMC ili kubeba mikoba ya Jackson Mayanja aliyefungashiwa virago vyake klabuni hapo.
Mayanja alipewa kandarasi ya mwaka mmoja iliyokuwa na kipengele cha kuongeza mkataba mwingine iwapo atakidhi masharti yaliyowekwa kwa kufuata falsafa za klabu hiyo jambo ambalo limekuwa gumu kwake kwa kile alichoeleza kutokuwa na washambuliaji halisia ndani ya kikosi na amefungashiwa jumla virago.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Djuma alisema kuwa kwa sasa yupo nchini Rwanda akiendelea na maisha yake kama kawaida kwani hana timu ya kufundisha baada ya kuachana na AS Kigali.
“Kwa sasa sina timu nipo naendelea na mambo yangu mwenyewe wakati ukifika nitajua jambo la kufanya kwani nilishaachana na AS Kigali, suala la KMC kwa sasa sina taarifa nalo ila kama itatokea tukafika maelewano nitafanya kazi kwani mimi ni kocha,” alisema Djuma.
Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa uongozi utaendelea na Kocha Mrage Kabange na Ahmady Ally mipango ya kumpata kocha ipo chini ya uongozi wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa.
Post a Comment