Upande wa utetezi kàtika kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ , jana Jumanne, Novemba 12, 2019 umelalamikia upande wa mashtakà kwa kuchelewesha upelelezi.
Kesi hiyo inamkabili dereva wa teksi, Mousa Twaleb, na wenzake wanne ambao bado hawajakamatwa. Wakili wa utetezi, Maufudhu Mbagwa, alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkúu Huruma Shaidi.
Alisema Septemba 16 mwaka huu upande wa mashtaka uliomba kupatiwa hati za kukamatwa kwa washtakiwa wengine na wao waliomba kupatiwa hati hizo lakini hawajapatiwa.
Alidai mwaka mmoja sasa umeshapita tangu mteja wake awe mahabusu na hawajaambiwa hatua ya upelelezi waliyofikia. Hakimu àlihoji sababu ya upande wa mshtakiwa kuharakisha kumshtaki mshtakiwa huyo wakati washtakiwa wengine bado hawajakamatwa.
Alieleza kama upande wa mashtaka wanaweza kuendelea na mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyo kwa upande wake, ufanye hivyo kuliko kuleta hati ya mashtaka ya watu wengi ambao hawajulikani watakamatwa lini.
Wakili wa serikali, Glory Mwenda, alidai kufuatilia suala hilo na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo ambapo ilipangwa Novemba 25 mwaka huu. Watuhumiwa wengine ambao upande wa mashtaka inawatafuta ni raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wanaodaiwa kumteka mfanyabiashara huyo.
Washtakiwa hao ambao ni Phila Tshabalala, raia wa Afrika Kusini; Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior, wote raia wa Msumbiji.
Katika kesi hiyo inadaiwa Mei Mosi na Oktoba 10, 2018, katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini, kwa makusudi, washitakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu.
Pia inadaiwa Oktoba 11, mwaka jana maeneo ya Hoteli ya Colloseum wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO kwa nia ya kumhifadhi kwa siri na kumweka maeneo ambayo ni hatari.
Pia inadaiwa Julai 10, mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha fedha ambazo ni Sh 8,000,000 wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.
MO alitekwa nyara Oktoba 11, mwaka jana alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huohuo katika eneo la Gymkhana jijini Dar es Salaam
Post a Comment