Bondia mmoja wa nchini Australia, Dwight Ritchie amefariki mara baada ya kutoka kwenye mazoezi.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27, na baba wa watoto watatu alikuwa ana mapambano na Michael Zerafa huko Melbourne.
"Ni maskitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanamisumbwi Dwight Ritchie ambaye amefariki akiwa anafanya kitu ambacho anakipenda," alisema promota wake Jake Ellis.
Ritchie alishindwa mara mbili katika mapambano 21, Hivi karibuni alipigana na Tim Tszyu wakiwa wanawania michuano ya uzito wa juu nchini Australia mnamo mwezi Agosti.
Kifo cha bondia huyo kimetokea mwezi mmoja baada ya kifo cha bondia wa Marekani kutokea.
- Bondia mwengine aaga dunia baada ya pigano kusitishwa
- Bondia aliyepigwa Knockout afariki
- Bondia mashuhuri Tanzania Mashali afariki
Bondia wa Marekani alikufa baada ya kupata jeraha kwenye ubongo mara baada ya kupigana na bondia Charles Conwell.
"Dwight atakumbukwa katika ulimwengu wa ndondi kutokana na kipaji chake na jinsi alivyokuwa akishiriki mchezo huo kwa namna ya kipekee na hata mfumo wake wa maisha."
Ritchie aliposhindwa mchezo uliopita ndio sababu iliyomfanya kurejea kupambana na Tommy Browne.
Kifo chake kimepokelewa na salamu ny
Post a Comment