DIDIER Deschamps Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa amethibitisha kuwa hatamuita Karim Benzema kipindi chake chote cha ukocha wa taifa hilo.

Straika huyo anayekipiga Real Madrid hajaichezea timu ya taifa tangu 2015 baada ya Deschamps kuamua kumpotezea kufuatia mgogoro na mchezaji mwenzake, Mathieu Valbuena.

Benzema akiwa na genge lake alipatikana na hatia ya kumfanyia uhuni Valbuena wa kutaka kumchomoa fedha kiujanja ili wasivujishe siri zake.

Benzema ameendelea kuwa mchezaji muhimu ndani ya Madrid ameshinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na moja la La Liga. 


"Uamuzi wa kuhusu Benzema ulikuwa ni wa kimichezo. Sidhani kama kurudi kwake kutaleta tija ndani ya timu ya Ufaransa," amesema Deschamps.

Benzema alimtuhumu Deschamps 2018 kuwa hamuiti kutokana na asili yake ya Algeria lakini Deschamps alisisitiza kuwa maamuzi yake ni sababu ya mpira.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.