Emmanuel Amuneke ametangaza kuwa yuko tayari kupokea ofa ya kazi mpya, miezi minne baada ya kuacha jukumu la ukufunzi wa timu ya taifa ya Tanzania baada ya kuafikiana na nchi hiyo.

Kocha huyo wa miaka 48 aliiongoza Taifa Stars kufuzu kwa mara ya kwanza katika kombe la mataifa ya Afrika tangu mwaka 1980, lakini timu hiyo iliondolewa katika mashindano hayo katika awamu ya makundi baada ya kumaliza ya mwisho kwenye kundi lao.

Mchezaji huyo wa mwaka wa Afrika, 1994, aliwahi kuwa msimamizi wa timu ya vijana wa nchi yake na klabu ya SC Khartoum, sasa anatafuta mwanzo mpya.

"Niko tayari kuchukua nafasi yoyote itakayotokea kwasababu wiki chache zilizopita nimejifunza mawazo mapya na njia ya kufikia mawazo hayo," Amuneke aliambia BBC Michezo akiwa nchini Uhispania.

"Kama meneja unahitaji kuwa mkweli na nafasi yako japo Tanzania ukurasa niliufunga, nilijifunza mengi katika kazi hiyo.

Iwe ni Afrika ama mahali popote nafasi itapatikana, unahitaji kuwa tayari kwasababu ni kitu unachotaka na kukiamini

"Nataka kuanza upya na iwe kitu cha uhakika, natumai malengo yangu yatatimia."

Baada ya kupata umaarufu katika soka ya bara Afrika, Amuneke amehusishwa na kazi nchini Nigeria siku zijazo kwa mujibu wa ripoti chombo kimoja cha habari.

Licha ya kuachana na majukumu yake mawili Afrika Mashariki, kufuatia maelewano ya pande mbili, mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona na klabu ya Sporting ya Ureno hana mpango wa kujidhibiti katika soka ya bara Afrika pekee.

Amuneke aliiongoza Taifa Stars (pichani) kufuzu kwa mara ya kwanza katika kombe la mataifa ya Afrika tangu mwaka 1980

"Lazima tuwape heshima wale ambao wanashikilia nyadhifa za ukufunzi nchini Nigeria na kwengineko. Binafsi, natazamia nafasi nyingine kwa matumaini makubwa," alisema.

"Iwe ni Afrika ama mahali popote nafasi itapatikana, unahitaji kuwa tayari kwasababu ni kitu unachotaka na kukiamini."

Amuneke alikuwa kocha msaidizi wakati Nigeria iliposhinda kombe la dunia Fifa kwa wachezaji walio chini ya miaka 17 kwa mara nne mtawalio katika Umoja wa Falme za Kiarabu mwaka 2013.

Miaka miwili baadae, aliongoza timu ya Nigeria ya wachezaji walio chini ya miaka 17 kwa mara ya tano kuwania kombe la Dunia lililoandaliwa nchini Chile.

Baada ya kujipambanua kama mkufunzi mahiri wa vijana, alipandishwa cheo kuwa kocha wa wachezaji walio chini ya miaka 20 inayojulikani kama Flying Eagles.

Kama mchezaji, alikuwa kiungo muhimu katika timu ya Super Eagles, kwa kufunga mabao yote ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1994, nchini Tunisia ambapo Nigeria iliishinda Zambia mabao 2-1 na kuchukua nafasi ya pili ya taji hilo la Afrika.

Pia aliiwakilisha timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles katika kombe la Dunia la mwaka 1994, na kufunga mabao ya kusisimua dhidi ya Bulgaria na Italia.

Miaka miwili baada ya ushindi wa Tunisia, alifunga tena bao la ushindi baada ya Nigeria kuifunga Argentina 3-2 katika fainali ya mwaka 1996 ya mashindano ya soka ya Olympiki mjini Atlanta na kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda dhahabu ya Olympiki.

Imeandaliwa na BBC

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.