Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amepigilia msumari kuondolewa kwa Kocha Mwinyi Zahera baada ya kufanya vibaya.
Akilimali ameliambia Spoti Xtra kuwa uongozi umefanya jambo sahihi kumuondoa kocha huyo japokuwa walitakiwa kuwa na umoja katika maamuzi kwa kuwa wanachama na mashabiki wamegawanyika katika suala hilo.
“Zahera alistahili kuondoka ndani ya Yanga kwani kibaya zaidi ambacho amekifanya ni hili la kutaka fedha zote za usajili apewe yeye na kweli jambo hilo lilifanyika na wachezaji amesajili mwenyewe.
“Lakini cha kushangaza timu hadi sasa haina mshambuliaji hata mmoja inafungwa tu na wala katika suala la kumalizia hakuna na wachezaji amewaleta mwenyewe, nashangaa anavyolalamika juu ya kuondolewa, timu hizi zina utashi wake zote za Simba na Yanga huyu akisema hivi na yule akisema vile basi watu wanafuatisha.
“Kinachotakiwa ndani ya timu ni kuwa na umoja ambao utasaidia kuwaweka watu pamoja kwani hadi sasa watu wametofautiana kuna wanaokubaliana Zahera aondoke na wale wanaopinga, watu wengi wamenitumia meseji,” alisema mzee Akilimali ambaye hivi karibuni aliipiwa deni la matibabu na Zahera.
Post a Comment