Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefutwa kazi baada ya kuongoza timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18.
Raia huyo wa Uhispania , ambaye awali alikuwa mkufunzi wa Paris St-Germain katika ligi ya Ufaransa na kushinda mataji matatu ya Yuropa akiwa na Sevilla, aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Arsenal mwezi Mei 2018, akimrithi Arsene Wenger.
Mahala pake patachukuliwa kwa muda mfupi na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Freddie Ljungberg.
Arsene Wenger akubali kuondoka Arsenal
Wenger: Sina wasiwasi wa kufutwa kazi
Arsene Wenger: Nililazimishwa kuondoka Arsenal
Arsenal inasema kwamba uamuzi huo ulichukuliwa baada ya matokeo ya timu hiyo kushindwa kufikia kiwango kilichohitajika.
Arsenal haijashinda katika mechi saba na ilipoteza 2-1 nyumbani dhidi ya klabu ya Ujerumani Eitracht Frankfurt katika ligi ya Yuropa siku ya Alhamisi.
Hakimiliki ya Picha @OptaJoe@OPTAJOE
Arsenal ilianza msimu huu wakirekodi misururu ya ushindi dhidi ya Newcastle na Burnley, lakini ushindi huo ulimalizwa baada ya kulazwa na Liverpool, kabla ya kurekodi sare mbili dhidi ya wapinzani wao wa London Tottenham na Watford.
Ushindi wao wa mwisho katika ligi ya Uingereza ulikuwa dhidi ya Bournemouth.
Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Freddie Ljunberg wa pili kushoto ndiye naibu wa Emery katika klabu hiyo
Siku ya Jumamosi, walitoka sare ya 2-2 ikiwa ni ya sita msimu huu nyumbani dhidi ya Southampton, huku Alexander Lacazette akifunga goli la kusawazisha katika muda wa majeraha.
Emery ni mkufunzi wa tatu kufutwa kazi katika ligi ya England msimu huu baada ya Javi Gracia na Mauricio Pochettino.
Ushindi wa mwisho wa Arsenal ulijiri dhidi ya Vitoria Guimaraes katika ligi ya Yuropa tarehe 24 mwezi Oktoba , ambapo walihitaji mipira miwili ya adhabu kupata ushindi wa magoli 3-2.
Ljungberg ameanza kuiongoza katika mazoezi timu hiyo na taarifa ya Arsenal ilisema: Tuna matumaini na Freddie Ljunberg kutuogoza. Usakaji wa kocha mpya unaendelea na tutatoa tangazo tutakapokamilisha mpango huo.
Siku ya Jumatano , BBC Sport iliripoti kwamba Arsenal inamuona Mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo kama mrithi wa Emery.
Majina mengine yanayohusishwa na tangazo hilo ni pamoja na mkufunzi wa zamani wa Tottenham, Pochettino naibu kocha wa Manchester City Mikel Arteta na mkufunzi wa zamani wa Juventus Massimiliano Alegri na Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe.
Walianza msimu huu baada ya kugharamika zaidi ya £130m walipomsaini winga Nicolas Pepe, beki wa katikati David Luiz, Beki wa kushoto Kieran Tierney, mshambuliaji Gabriel Martinelli na beki William Saliba, ambaye atajiunga msimu ujao.
Pia klabu hiyo ilimununua kwa mkopo kiungo wa kati Dani Ceballos kutoka Real Madrid.