2019


Kaimu kocha mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amelazimika kutolea ufafanuzi wa kiwango cha timu yake kilichooneshwa katika mchezo dhidi ya Biashara United Desemba 30 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao wengi wanautumia kama picha halisi ya kiwango cha Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Simba Januari 4, wengi wameponda kiwango cha Yanga kupata ushindi wa tabu wa goli 1-0 lililofungwa na Tariq Seif dakika ya 83 dhidi ya Biashara United.

“Kabla ya kucheza tumekuwa na safari ndefu kama mnakumbuka kabla hatujacheza mechi yetu Mbeya tulikuwa na wastani wa safari ya saa 18 na kurudi kuwa ilitubidi tuondoke ghafla kwa sababu ya mechi ya Iringa ambayo hatukuwa na program nayo kwa hiyo baada ya mechi ikatubidi tuondoke usiku tena kwa sababu tuna mechi leo” amesema.

“Kwa hiyo ile kukatakata safari na nini kuna kuwa na ile uchovu, kuna kauchovu flani kalikuwepo lakini naamini kama tungekuwa katika kiwango chetu bora au tusingekuwa na uchovu tungepata matokeo mazuri tena mapema zaidi game ilikuwa tumeshaimaliza mapema” amesema.

Licha ya kauli hiyo ya Mkwasa kueleza kuwa ni uchovu, hofu ya mashabiki inatajwa kuwa inatokana na kiwango cha timu yao katika mechi 5 zilizopita ni mechi moja tu ndio imepata ushindi wa zaidi ya goli moja (3-2 vs JKT Tanzania) lakini mingine imekuwa ikipata ushindi wa goli 1-0 au sare ya 0-0, katika mechi hizo Yanga imefunga jumla ya magoli 6 na kufungwa 2


UONGOZI wa Yanga kwa kushirikiana na mabosi wa GSM, umekamilisha dili la mshambuliaji Ykipe Gnamien kwa kumpa dili la miaka miwili.

Habari zinaeleza kuwa licha ya danadana za awali kwa mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coas aliyevunja mkataba na Gormahia mwenye mwili jumba kwa sasa kila kitu kimekwenda sawa na Yanga.

"Tayari ameshapewa kibali na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) na yupo kwenye hesabu za kuivaa Simba, Januari,42020," ilieleza taarifa hiyo kutoka ndani


SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mashabiki wasiwe na haraka ya kupata matokeo makubwa kwani kazi ndo kwanza inaanza.

Kocha huyo aliyepokea mikoba kutoka kwa Patrick Aussems ameiongoza Simba kwenye mechi tatu na kukusanya jumla ya mabao 12 ambapo alianza kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Arusha FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho na alishinda mabao 4-0 dhidi ya Lipuli na mbele ya KMC aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ilikuwa ni mechi za ligi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.

"Bado kikosi kinaimarika taratibu na wakati ukifika kila mmoja atapenda kuona namna timu inavyopambana na kufikia mafanikio ambayo tunayahitaji," amesema.

Simba ni kinara ndani ya ligi akiwa na pointi 31 na amecheza jumla ya mechi 12, kesho atapambana na Ndanda FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Uhuru.


Mrembo wa Kirusi mwenye mvuto wa aina yake, Viktoria Odintcova, amedai kuwa aliikaushia na kuifutilia mbali meseji aliyotumiwa na supastaa Cristiano Ronaldo baada ya fowadi huyo wa Juventus, kumtumia ujumbe Instagram.

Mrembo huyo, 34, mwenye wafuasi milioni tano kwenye Instagram, amefunguka kuwa aliitosa meseji ya staa huyo miezi kadhaa iliyopita.

“Aliniandikia ujumbe mfupi. Ilikuwa ni zamani kidogo. Aliandika hivi, “Mambo, mzima wewe?”

“Nilifuta meseji hiyo na sikujibu,” alisema mrembo huyo.

Aliongeza: “Sikutaka kumpa nafasi, kwa sababu nawajua wanawake wengine aliowaandikia, kwa hiyo nilielewa lengo lake mapema.”

Ronaldo kwa sasa yupo penzini na mrembo Georgina Rodriguez tangu 2016 na wana mtoto mmoja wa kike pamoja aitwaye Alana


KUELEKEA Mtanange wa kukata na shoka mnamo Januari 4,2020  kati ya watani wa jadi Simba na Yanga Kampuni  ya GSM Group ambao ni moja ya wadhamini wakuu wa timu ya Yanga kupitia Godoro la Chapa GSM inatarajia kutoa zawadi ya godoro la nchi 5x6x8 kwa mchezaji wa Yanga atakayeibuka nyota wa mchezo baina yao na Simba.

Pambano hilo la kukata na  shoka ambalo ni la kwanza msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, litachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam leo Desemba 30, 2019, Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu, amesema wameamua kutoa zawadi hiyo ili kuwapa morari wachezaji wa Yanga.

Amesema wao kama wadhamini wa Yanga ni wajibu wao kuhakikisha timu hiyo inawapa raha mashabiki wake kwa kushinda mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla. 


"Kuelekea mechi ya kukata na shoka kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga, moja ya wadhamini wakuu wa timu ya Yanga, GSM Group kupitia godoro chapa GSM, tutatoa zawadi nono kwa mchezaji bora wa timu ya Yanga wakati wa mechi Yanga  na Simba kwa  kumzawadia godoro la nchi 5x6x8. 

 "Tunaamini zawadi hii itawaongezea wachezaji morali ya kupambana kuiwezesha Yanga kupata ushindi na hivyo kuwapa raha mashabiki wao na kuendelea kupata matokeo chanya kwa mechi zingine zijazo.

Aliongeza: "Yanga ni klabu kubwa na bora hapa nchini kama ilivyo kwa magodoro yetu Chapa GSM hivyo mashabiki wao nao wanastahili matokeo yaliyo bora uwanjani ndio maana tumeamua kutoa zawadi ili kuwapandisha mzuka wachezaji wa Yanga kuelekea mchezo huo muhimu wa Jumamosi ya Januari 4." 


Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliishukuru GSM Group kwa ahadi hiyo ambayo anaamini itawaongezea hamasa wachezaji wa timu yao.


BIASHARA United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza kutoka mkoani Mara walibakiza dakika sita tu kuambulia pointi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga uliocchezwa uwanja wa Taifa ila bahati haikuwa yao walipoteza.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Tariq Seif dakika ya 84 akimalizia pasi ya nahodha Papy Tshishimbi akiwa ndani ya 18 na kuzamisha moja kwa moja wavuni.

 Seif ambaye aliwahi kucheza Biashara United kabla ya kusajiliwa hivi karibuni kwenye dirisha dogo ndani ya Yanga akitokea nchini Misri amesema kuwa anaona fahari kuipa pointi tatu, timu yake.

"Nimefurahi kuona nimeipa ushindi timu yangu inaamanisha kwamba ninaweza na nitaendelea kupambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuwa bora zaidi," amesema.

Yangaimecheza jumla ya mechi 11 inafikisha jumla ya pointi 24 sawa na Kagera Sugar inakuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa ikiwa nyuma ya Simba walio kileleni wenye pointi 31 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 12

ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC, leo anangia kikaangoni tena baada ya kupoteza mechi yake ya pili akiwa kwenye benchi la ufundi ndani ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0 na Coastal Union ya Tanga.

Leo atakutana na timu ya Polisi Tanzania iliyotoka kushinda mabao 2-1 mbele ya KMC uwanja wa Ushirika, Moshi.

Mechi ya kwanza kwa Cioaba ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting ambayo alikuwa ugenini na alifungwa bao 1-0 mchezo wake wa pili kupoteza ilikuwa mbele ya Coastal Union alifungwa pia bao 1-0 uwanja wa Mkwakwani.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa umakini ulikosekana katika kumalizia nafasi za mwisho.

“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila timu inapambana kupata matokeo ila nina amini tutafanya vizuri kwenye mechi zetu zinazofuata,” amesema Cheche


Katika kuhakikisha kiungo Haruna Niyonzima anauwahi mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, uongozi wa Yanga umepanga kumpandisha ndege mmoja wa viongozi kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya kufuatilia Kibali cha Uhamisho wa Kimataifa (ITC) cha mchezaji huyo fundi.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Januari 4, mwakani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu hiyo. Niyonzima ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuwepo katika mchezo huo baada ya kusajiliwa hivi karibuni na kupewa mkataba wa miaka miwili akitokea AS Kigali ya Rwanda.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mabosi hao wamepanga kusafiri ndani ya wiki hii kwenda Rwanda kwa ajili ya kufuatilia kibali hicho kutoka kwenye Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa). Aliongeza kuwa viongozi hao wanaamini uwepo wa kiungo huyo

mwenye uwezo mkubwa wa kuchezesha timu na kupiga pasi za mwisho utakiimarisha kikosi chao kutokana na uzoefu alionao. “Viongozi wanataka kumuona Niyonzima akijiunga na kambi haraka mara baada ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Biashara United.

“Hivyo, mmoja wa viongozi atakwenda Rwanda kuhakikisha masuala ya ITC yake yanamalizika haraka kwani hiyo ndiyo inamchelewesha kuja nchini kujiunga na timu,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza kuwa. “Kiungo huyo tayari ameandaliwa nyumba atakayofikia kwenye ‘apatmenti’ za Shekilango alipokuwa anakaa aliyekuwa mshambuliaji wetu Urikhob (Sadney).

” Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alikazia ujio wa Niyonzima kwa kusema wanatarajia kumpokea hivi karibuni ili kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria. “Niyonzima ameomba kucheza mchezo wa mwisho na timu yake ya AS Kigali, kisha ndio afanye safari ya kuja Bongo tayari kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata  na uongozi umekubaliana naye. “Kuna vitu vichache tu ndivyo vilivyobaki kwa ajili ya kukamilisha usajili wake,” alisema Bumbuli. Wilbert Molandi na Khadija Mngwai,


Katika kuelekea mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba, matajiri wa Yanga, Kampuni ya GSM ambao ndiyo wadhamini wa timu hiyo wamewalipa wachezaji wote wanaodai fedha za usajili. Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Januari 4, mwakani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kabla ya wachezaji hao kulipwa stahiki zao, hivi karibuni GSM ilifanya balaa katika usajili kwa kusimamia usajili wa nyota kadhaa akiwemo Haruna Niyonzima.

Hiyo ikiwa ni siku chache mara baada ya wachezaji kulalamika kwenye mitandao ya kijamii wakidai kuwa hawathaminiwi kutokana na kutolipwa fedha zao za usajili kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mabosi hao wamelipa stahiki hizo kwa wachezaji katika kuwapa morali kuelekea pambano lao dhidi ya Simba.

Mtoa taarifa aliwataja wachezaji hao waliolipwa stahiki zao ni Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Said Juma ‘Makapu’, Juma Abdul, Juma Mahadhi, Andrew Vincent ‘Dante’ na Ramadhani Kabwili.

Aliongeza kuwa, wachezaji hao wamelipwa madai yao juzi, huku wakipanga kuwalipa mishahara ya mwezi huu wa Desemba wiki hii hiyo o yote katika kutengeneza morali ya wachezaji.

“GSM wamepania kuifanyia makubwa timu katika kuelekea mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba, hivyo tayari jana (juzi) wamewalipa wachezaji wote waliokuwa wanadai fedha za usajili.

“Kati ya hao yupo Ngassa ambaye hivi karibuni alionekana kulalamika kwenye mitandao ya kijamii pamoja na Dante mwenyewe ambaye amerejea kikosini.

“Kikubwa GSM wanataka kuona hujuma na mipango wanayotaka kuwatumia wapinzani wao Simba hazifanikiwi na ndiyo maana wamewalipa wachezaji hao huku wakipanga kuwalipa mshahara wa mwezi huu wiki ijayo,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa Ofi sa Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo, alisema kuwa: “Hilo suala lipo kwa viongozi wa juu lakini kama umelipata basi itakuwa kweli, kwani viongozi hivi sasa wamepanga kufuta madeni yote ambayo tunadaiwa na wachezaji.”


Washindwe wenyewe sasa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Simba juzi Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Simba walipewa zawadi ya Krismasi na timu yao hiyo pendwa, ulitengeneza njia nyeupe kwa Simba kuelekea kuutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara waliouchukua mara mbili mfululizo kutokana na ratiba kuwa rafi ki zaidi kwao kuliko watani zao wa jadi, Yanga.

Simba ilianza kujipatia bao lake la kwanza kupitia kwa Francis Kahata aliyefunga dakika ya 10 akimaliza pasi ya Shomary Kapombe. Dakika ya 49, Meddie Kagere aliongeza bao la pili akiunganisha pasi ya Clatous Chama.

Hassan Dilunga akafunga kwa penalti dakika ya 57, kisha Dilunga akafunga hesabu dakika ya 64 baada ya kupokea pasi safi  kutoka kwa Sharaf Shiboub.

Kwa sasa njia ya ubingwa kwa Simba ni nyeupe kwani wapinzani wao wa jadi, Yanga ambao wamekuwa wakitamba kwamba watawaharibia, juzi Jumanne walisuluhu na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine ambao walikuja kuulalamikia kwamba haukuwa rafi ki kwao.

Sasa kesho Ijumaa tena Yanga itakuwa Sokoine kucheza na Prisons, kama mambo yakiwa vilevile vibaya, basi Simba itazidi kuwaacha mbali sana kwani hivi sasa mabingwa hao watetezi wapo kileleni na pointi zao 28.

Yanga inazo 18. Tofauti yao ni pointi kumi ambapo Simba imecheza mechi 11 na Yanga 9. Ikumbukwe kuwa, timu hizo zitakuja kupambana Januari 4, mwakani, lakini kabla ya kukutana, Simba itakuwa na michezo miwili jijini Dar ambayo itacheza kwenye uwanja saaafi  usiokuwa na visingizo vya kukosa matokeo, huku Yanga ikiwa na mechi moja Mbeya kwenye uwanja korofi , kisha nyingine Uwanja wa Uhuru ambao upo katika hali nzuri. Simba itacheza na KMC na Ndanda, huku Yanga ikicheza na Prisons na Biashara United


Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umepanga kutuma barua kwenda Bodi ya Ligi ya Tanzania (TPLB) ili kurejeshewa gharama walizozitumia kuelekea mechi yao na Tanzania Prisons.

Taarifa zinasema kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli, ameeleza wamekuwa wakitumia fedha nyingi wanaposafiri kwenda ugenini.

Maamuzi ya Yanga kutaka kufanya hivyo ni kutokana na bodi hiyo kubadilisha uwanja wa kuchezea kutoka Sokoine Mbeya ambao umehabribiwa na tamasha la muziki lililofanyika juzi kwenda Samora Iringa.

Kutokana na mabadiliko hayo, Yanga wameeleza kuwa utawaingiza kwenye hasara lakini akisema pia watapambana kugharamika sababu wanapigania ubingwa


KOCHA wa Tanzania Prisons, Mohammed ‘Adolf’ Rishard, amesema hawatakubali rekodi yao ya kutokufungwa kwenye Ligi Kuu ivunjwe na Yanga kwenye mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Tanzania Prisons ambayo imecheza michezo 13 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 na ikiwa imeshinda mechi tano, sare michezo nane, inakutana na Yanga inayoshika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 18.

Adolf Richard ametoa tahadhari hiyo kwa Yanga ikiwa ni siku moja baada ya kupunguzwa kasi kwa kugawana pointi na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja Sokoine ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho.

“Tumejijengea falsafa moja ya kuwaheshimu wapinzani na tutaindeleza kwa Yanga ila wasije wakatarajia watakuja kupata matokeo kirahisi.

"Baada ya kutoka sare mechi iliyopita hatuwezi kukubali rekodi ya kutokufungwa ivunjwe na Yanga tena katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.

Alisema wanaiheshimu Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazoefu na wenye uwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote, lakini kupitia mechi iliyopita wameona udhaifu wao mwingi, hivyo wamejipanga kuhakikisha dakika 90 zitaamua mshindi kuwa wao.

“Wachezaji wote wako fiti kwa mchezo, kikubwa tubaomba mashabiki wa Mbeya na sehemu za jirani kujitokeza kwa wingi kutushangilia kwani ushindi wetu ni sifa ya mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini,” alisema Adolf Richard.

Alipotafutwa kocha wa Yanga, Charles Mkwasa, kuzungumzia maandalizi ya mchezo dhidi yaTanzania Prisons, aligoma kuzungumza kwa madai yupo kwenye mapumziko ya sikukuu ya Krismasi.

“Kama unataka taarifa kuhusu maandalizi ya timu kujipanga na mchezo ujao mtafute Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, atakuambia lakini kwa sasa nimechoka na sitaki kuongelea maana nipo mapumziko nasheherekea sikukuu ya Krismasi hapa Mbeya,” alisema Mkwasa


ALIWAHI kutokea bwana mmoja aliyekuwa maarufu sana duniani katika miaka ya 1975, huyu jamaa aliitwa Arthur Ashe, mcheza tenisi wa Marekani aliyepata umaarufu mkubwa kwa kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu hasa wale wenye asili ya Afrika, huyu jamaa aliwahi kusema hivi: “Success is a Journey, Not a Destination”, alimaanisha “Mafanikio ni safari na sio mwisho.”

Nimependa kuanza na bwana Ashe kwani maneno yake ndio msingi wa makala haya yanayomuangazia kiungo mshambuliaji hatari wa KMC, Hassan Kabunda, akitueleza changamoto kubwa alizowahi kukutana nazo katika maisha yake ya soka.

TUANZE NA HISTORIA YAKO KWA UFUPI

“Naitwa Hassan Salum Kabunda mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Salum Kabunda ‘Ninja’, kiufupi maisha yangu ya soka niliyaanzia katika kituo cha kukuzia vipaji cha DYOC jijini Dar, na baadaye nilielekea Ashanti Utd, ambako nilicheza kisha nikaenda Mwadui ya Shinyanga na mwaka 2018 ndiyo nikasajiliwa KMC ambako niko mpaka sasa.”

Zifuatazo ni changamoto kubwa alizowahi kukutanana nazo Hassan Kabunda;

AWEKWA BENCHI MECHI NANE KISA ZENGWE LA MWALIMU

“Unajua katika mpira unaweza kukutana na kocha akawa hakuelewi kabisa hata ufanye nini kiasi anaweza akakuweka benchi au hata kukutoa kwa mkopo na hili liliwahi kunitokea mimi nikiwa Mwadui ambapo kocha wangu kipindi hicho, Ally Bizimungu, aliniweka nje ya uwanja mechi nane bila sababu yoyote ya msingi, jambo ambalo lilinipa wakati mgumu sana kiasi cha kuniondolea hali ya kujiamini uwanjani.”

ASHUSHWA KWENYE BASI SAA TISA USIKU WAKIWA WANAELEKEA KWENYE MECHI

“Tukio lingine ambalo siwezi kulisahau ni lile la kushushwa kwenye basi la timu (akiwa Mwadui FC) saa tisa usiku tukiwa tunajiandaa na safari ya kwenda kucheza na Azam, eti kwa sababu watu waliokuwa wanaenda kucheza mechi walikuwa wamezidi, nakumbuka kocha Julio alikuwa anataka mimi nisafiri ila viongozi wakakataa, huwezi amini ilinibidi nishuke tu.”

APOKEA KIPIGO BAADA YA KUPIGA HAT-TRICK FAINALI

“Unajua mimi napenda sana mpira na mapenzi ya soka yalinipa wakati mgumu sana utotoni kwani nilikuwa napigwa sana na mama kwa sababu alikuwa akinikataza kucheza mpira na watu wakubwa akihofu wangeniumiza, sasa kwa ubishi wangu nakumbuka siku moja nilitoroka na kwenda kucheza mechi ya fainali ya ‘chandimu’ nikiwa naumwa, nikafanikiwa kufunga hat-trick kwenye mchezo huo ambao uliisha kwa sisi kushinda 4-2, basi ikawa shangwe pale tukafurahia sana ushindi, sasa ile kurudi nyumbani nikapokea kipigo kizito kutoka kwa mama lakini sikuacha kucheza kwa kuwa naupenda sana na uko kwenye damu.

“Hilo ni moja kati ya matukio mengi sana ya kupigwa kwa sababu ya mpira nakumbuka mama alikuwa akinipiga sana mpaka ikafika wakati akachoka na kuamua kunikabidhi kwa mjomba basi ilikuwa hatari mzee.”

ISHU YA MALIPO JE?

“Hapo kaka umegusa penyewe, unajua soka letu lina changamoto nyingi sana hasa linapokuja suala la malipo, nadhani unasikia hata Simba na Yanga jinsi changamoto hiyo ilivyo kubwa, suala linalopelekea usipokuwa mvumilivu unaweza hata kubeba mabegi yako na kurudi nyumbani, kwa mfano mimi binafsi Mwadui mpaka sasa naidai pesa yangu ya usajili, hivi ninavyokuambia nipo kwenye mchakato wa kupeleka madai yangu TFF ili kudai haki yangu kwani lile ni jasho langu.”

MATIBABU TATIZO HAPA NCHINI

“Unajua majeraha kwa mchezaji ni kawaida, ila changamoto huja katika suala la huduma za matibabu ambazo kwa kweli zina changamoto, na kwa upande wangu sikumbuki ni lini ila nakumbuka niliwahi kupata majeraha ya nyama za paja mazoezini tukiwa tunajiandaa na mechi kesho yake ambayo yaliniweka nje kwa muda mrefu kidogo na hili likichangiwa na huduma duni za kiafya kwa wachezaji.

“Nadhani hata wewe unaona kuna tofauti kubwa ya kwetu na wenzetu walioendelea kiasi kwamba huku kwetu kuna baadhi ya watu wamelazimika kuacha mpira kutokana na kushindwa kupata matibabu stahiki ya majeraha yao.”

NINI USHAURI WAKO KWA VIJANA WENYE MALENGO YA KUFANIKIWA KUNAKO SOKA?

“Kwanza niseme kuwa unapotaka kufanya jambo lolote lazima ujue utakutana na changamoto hivyo vijana wanaokuja kwenye soka wanapaswa kujitahidi sana kuwa wavumilivu, waachane na makundi potofu na starehe zisizo na mpango na wawekeze nguvu zao nyingi katika mazoezi, kuwa na heshima na zaidi sana wamweke Mungu mbele.”

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.