Zahera alisema atampa mechi hizo mfululizo kwani anaamini ni mchezaji mzuri ambaye atafanya vyema kwenye timu yake.


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema atampa mechi tano mfululizo straika wake, David Molinga ‘Ndama’ ili kiwango chake kiendelee kuwa imara.

Molinga alicheza mechi ya kwanza juzi Jumatano tangu asajiliwe na timu hiyo ambapo alimpa dakika zote 90 za mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambapo walifungwa bao 1-0.

Zahera alisema atampa mechi hizo mfululizo kwani anaamini ni mchezaji mzuri ambaye atafanya vyema kwenye timu yake.

“Siku mbili kabla ya kukamilisha usajili wa Ligi Kuu, nilipata taarifa kuwa Molinga anamaliza mkataba na timu yake ya zamani kwa vile nilikuwa namfahamu niliamini anaweza kuwa bora na kuisadia Yanga msimu huu,”

“Wakati tunakamilisha utaratibu wa usajili wake tena siku ya mwisho Molinga hakuwa anafanya mazoezi kwani alikuwa mapumziko baada ya kumaliza kucheza ligi na ameongezeka uzito, tulimsajili na anaendelea kufanya mazoezi ya mwili huku ligi ikiwa inaendelea.

“Tangu amekuja nchini mpaka sasa amepunguza kilo tano, naamini nikimpa mechi nyingine tano mfululizo za kimashindano na ratiba yake ya mazoezi ngumu anayoifanya atakuwa bora na hata hao wanaombeza wataacha.

“Namfahamu Molinga, kabla ya kumleta hapa nchini naelewa katika uwezo wake na kama akianza kufanya kile ambacho nakifahamu akiwa DR Congo sioni sababu ya kushindwa kufunga mabao mengi kama ambavyo alikuwa akifanya Heritier Makambo msimu uliopita,” alisema Zahera.

Molinga alisema “Si muda wa kuangalia mashabiki wanasema nini kwani sijafuata hayo.”

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.