Sanchez alihitaji mechi 32 kufunga mabao matatu kwenye ligi, wakati James amefunga idadi hiyo kwenye mechi nne tu, na hivyo kuwa nyuma kwa mechi 28.

MANCHESTER, ENGLAND. MASHABIKI wa Manchester United wamemwaga sifa kama zote kwa staa wao mpya, Daniel James kwamba kinda huyo amemfundisha Alexis Sanchez namna nzuri ya kuichezea timu hiyo huko Old Trafford.
James ndio kwanza amecheza mechi nne tu kwenye Ligi Kuu England, lakini amefunga mabao matatu, ikiwa idadi sawa na aliyofunga Sanchez kwenye ligi hiyo kwa muda wote aliokuwa Man United kabla ya kupigwa kibuti cha mkopo kwenda Inter Milan.
Sanchez alihitaji mechi 32 kufunga mabao matatu kwenye ligi, wakati James amefunga idadi hiyo kwenye mechi nne tu, na hivyo kuwa nyuma kwa mechi 28. Kwa kasi hiyo ya James, mashabiki wa Man United wanamwona Sanchez alikuwa akiwaibia tu, hasa kutokana na mshahara wake aliokuwa akilipwa, Pauni 505,000 kwa wiki.
Shabiki mmoja aliandika kwenye Twitter: "Daniel James tayari ameshaonyesha kuwa ni mchezaji bora Manchester United kuliko Alexis Sanchez kwa muda wake wote aliokuwa klabuni."
Mwingine aliongeza: "Daniel James sasa amefunga idadi sawa ya mabao kwenye Ligi Kuu England, matatu kwenye mechi nne tu, kwa kulinganisha na Alexis Sanchez aliyofunga kwa miezi 18 kwenye timu."
Mashabiki wengine wanaamini kocha Ole Gunnar Solskjaer atakuwa amefanya usajili bora wa msimu kwenye kikosi hicho cha Old Trafford baada ya kumnasa kinda huyo kutoka Swansea City kwa ada ya Pauni 18 milioni.
Kuna shabiki ameandika hivi: "Daniel James, bila ya shaka ni usajili bora Man United katika kipindi cha miaka minne iliyopita au zaidi."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.