UONGOZI wa Yanga umesema kuwa itakuwa kazi ngumu kwa wapinzani wao Zesco kupenya uwanja wa Taifa kwani wamejipanga kumaliza mchezo mapema kutokana na hasira walizopewa na Simba pamoja na KMC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kutolewa kwa Simba mapema licha ya msimu uliopita kufanya vema kumewapa hasira ya kupambana ili kutinga hatua ya makundi.

"Kwa sasa tunajua kwamba Simba ameshatolewa kwenye michuano hii ya kimataifa pamoja na KMC kutolewa kwao kumetufanya tuwe na hasira ya kupambana kutafuta matokeo chanya kwenye michezo yetu.

" Kufanya kwetu vizuri kutaongeza pointi na idadi ya timu shiriki tukishindwa itakuwa pigo, mashabiki watupe sapoti nasi hatutawaangusha katika hilo kikubwa ni kuamini kwamba tunaweza," amesema Saleh.

Yanga itamenyana na Zesco, Septemba 14 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wao wa hatua ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.