KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mashabiki wa Yanga wasiwe na presha kwani michezo ya Ligi Kuu Bara ipo mingi watafanyia kazi makosa ambayo wameyafanya mbele ya Ruvu Shooting.

Akizungumza Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa anashangaa mashabiki wanaosema kuhusu kupoteza mchezo wa kwanza na kusahau kwamba kuna michezo mingi kwenye ligi.

“Ligi haina mchezo mmoja tukasema imemalizika hapana bado muda wa kufanyia kazi makosa upo na tutafanya vizuri michezo mingine ambayo imebaki ni suala la kusubiri tu.

“Mpaka sasa nimeshajua makosa yalipo kwa wachezaji mbali na uchovu ambao ulituponza bado tuna michezo mingi mkononi hiyo tutafanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu,” amesema Zahera.

Msimu huu Zahera amevunja rekodi aliyoweka msimu uliopita kwa kufungwa baada ya mchezo wa kwanza tofauti na msimu uliopita ambapo alipoteza baada ya kucheza michezo 19 amebakiwa na michezo 37 kufuta makosa yake.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.