KUELEKEA kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zesco unaotarajiwa kuchezwa Septemba 14 uwanja wa Taifa, tayari mlinda mlango, Farouk Shikalo amepata kibali cha kushiriki michuano ya kimataifa.

Shikalo ambaye amejiunga na Yanga akitokea timu ya Bandari alikosa michezo miwili ya kimataifa dhidi ya Township Roller na langoni alikaa Metacha Mnata jambo litakaloongeza ugumu wa namba ndani ya kikosi.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa utaratibu wa kukamilisha kibali kwa Shikalo umefikia hatua nzuri na wana imani ya kumtumia kwenye mchezo dhidi ya Zesco.

“Kwa sasa mipango inaendelea vema kuelekea mchezo wetu dhidi ya Zesco na tayari tumekamilisha hatua zote za kupata kibali rasmi cha kumtumia Shikalo kwani kila kitu kipo sawa.

“Kinachosubiriwa kwa sasa ni uthibitisho rasmi kutoka kwa Caf juu ya kumtumia mchezaji wetu Shikalo kwenye mechi ya marudio huku na wengine tukiendelea kufuatilia taarifa zao.” amesema Ten.

Wachezaji wengine ambao vibali vyao vinafuatiliwa na walikosa mchezo dhidi ya Township Rollers ni pamoja na David Molinga ‘Mwili Jumba’ na Maybin Kalengo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.