Wasaka vipaji wa Manchester United, wanadaiwa kuwa hivi karibuni walisafiri hadi Ulaya ya Mashariki kumuangalia kipa namba moja wa Dinamo Zagreb, Dominik Livakovic.
London, England. Wasaka vipaji wa Manchester United wameanza mchakato wa kumtafuta mapema mrithi wa kipa, David de Gea ambaye anaweza kuondoka, Januari.
Kipa huyo raia wa Hispania, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari amekataa ofa ya Pauni 350, 000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya kwa mujibu wa mtandao wa The Sun, uliopo England.
De Gea anaweza kuingia makubaliano ya kimkataba wa awali na klabu yoyote kuanza Januari.
Paris Saint-Germain imeripotiwa kufuatilia sakata la kipa huyo na Manchester United kwa ukaribu kutokana na kuhitaji kwao huduma ya kipa huyo huku wakiandaa kitita cha Pauni 30milioni.
Wasaka vipaji wa Manchester United, wanadaiwa kuwa hivi karibuni walisafiri hadi Ulaya ya Mashariki kumuangalia kipa namba moja wa Dinamo Zagreb, Dominik Livakovic.
Livakovic ni miongoni mwa makipa ambao wako kwenye orodha ya wachezaji ambao wanatazamwa kama mbadala wa De Gea, huku mwingine ni chaguo la kwanza la Atletico Madrid, Jan Oblak.
Pamoja na zoezi hilo kuendelea, pia kipa Dean Henderson ambaye ni mchezaji wa Mashetani Wekundu wa Old Trafford anayeichezea, Sheffield United, kwa mkopo naye anatazamwa kama ataweza kumudu nafasi hiyo.
Manchester United hawatakuwa na namna nyingine ya kumbakisha De Gea kama asiposaini mkataba mpya hadi Januari zaidi ya kumuuza ili asije akaondoka bure mwisho wa msimu huu.
Post a Comment