Yondani, ambaye aliichezea Simba kwa misimu sita kuanzia mwaka 2006 hadi 2012 kisha akatua Yanga, bado anacheza kwa kiwango bora na kuwa tegemeo hadi kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.
KWA mwonekano wake unaweza kudhani beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondan a.k.a Coton ni muhuni flani hivi, lakini asikwambie mtu nyuma yake ameficha siri kubwa inayomfamnya kuendelea kucheza kwa kasi na kiwango kile kile.
Siri hiyo ndio inayomfanya Yondani kuwepo panga pangua kwenye safu ya ulinzi ya Yanga akiunda kikosi cha kwanza licha ya kusajiliwa kwa mastaa wapya wa ndani na wa kigeni.
Kwa kifupi, kuna mastaa wanaopigania namba kweye jeshi la Mwinyi Zahera hasa kwenye usajili mpya msimu huu, lakini Yondani lazima achomoze na anapokosekana basi mashabiki hukosa imani.
Yondani, ambaye aliichezea Simba kwa misimu sita kuanzia mwaka 2006 hadi 2012 kisha akatua Yanga, bado anacheza kwa kiwango bora na kuwa tegemeo hadi kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.
Hata hivyo, makocha waliomfundisha Yondani kwa nyakati tofauti wamefunguka wakisema, sababu inayolinda kiwango chake ni Kilima cha Tatu kilichopo eneo la Malale huko Tuangoma nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kocha Kenny Mwaisabula ni kati ya watu wanaomfahamu Yondani nje ndani na anafichua, jamaa anafanya mazoezi binafsi zaidi ya yale anayopewa na kocha wanapokuwa na kikosi kizima.
Mwaisambula, ambaye anaishi jirani na Yondani, alisema kilima hicho kimekuwa siri ya mafanikio kwa beki huyo kutokana na kufanya mazoezi binafsi kwenye eneo hilo.
Alisema Yondani anapandisha na kushuka kwa kasi kwenye kilimo hicho kwa zaidi ya mara 20 na kwamba, kuna wakati yeye ndio humsaidia kuhesabu ruti hizo kisha anahamia kwenye mazoezi ya kuchezea mipira.
“Huyu Yondani ni jirani yangu hivyo, namfahamu vizuri sana. Kuna wakati akifanya mazoezi tunakuwa pamoja na ni mtulivu tofauti anavyochukuliwa kuwa ni mhuni.
“Yondani anaheshimu kazi yake, analinda kipaji chake kwa mazoezi na kama angekuwa mtu starehe asingeweza kufanya mazoezi kama hayo.
“Sijawahi kumshuhudia hata kwenye matamasha, nadhani hata mialiko ya kwenye starehe hajawahi kuonekana na siku zote ni mtu wa vitendo.
“Namfananisha na Juma (Kaseja), ambaye amejitunza kwa muda mrefu na sasa amerudi Taifa Stars.
“Huyu Yondani kuna kazi kubwa kumpora namba pale Yanga,” alisema.
Naye Kocha Athuman Bilali ‘Bilo’ alisema amemfundisha Yondan miaka ya nyuma akiwa na timu ya Chanel Afrika ambayo ni maarufu mkoani Mwanza, alisema siku zote hujitofautisha na wengine uwanjani. “Bado sijaona aina ya beki kama Yondani, zamani alikuwa Pascal Wawa wakati anacheza kwa Azam FC, lakini kwa sasa kabaki mwenyewe tu,” alisema.
Yanga imefanya usajili wa mabeki wapya ambao ni Lamin Moro, Ally Sonso na tayari wamecheza naye pamoja kwa baadhi ya mechi na Ali Ali, ambaye bado hawajaanza kucheza kwa pamoja.
Post a Comment