Lionel Messi ataruhusiwa kuondoka Barcelona bila malipo yoyote msimu ujao , iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atapendelea kufanya hivyo kutokana na kifungu cha sheria katika kandarasi yake. (El Pais, via L'Equipe)
Messi ataruhusiwa kuzungumzia hatma yake na klabu yoyote kutoka Januari mosi. (Marca - in Spanish)
Real Madrid itamwania mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe msimu ujao .
Mabingwa hao wa Ufaransa waliwaonya Barcelona kuhusu lengo hilo la Real Madrid wakati wa mazungumzo ya vilabu hivyo viwili kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu huu.. (Sport - in Spanish)
Mshambuliaji wa Brazil Neymar atalazimika kusalia PSG hadi pale atakapokubali kupunguza marupurupu yake kulingana na rais wa La Liga Javier Tebas. (Mail)
Chris Smalling yuko tayari kuondoka Man United baada ya beki huyo mwenye umri wa miaka 28 kujiunga na klabu ya Roma kwa mkopo. (Mirror)
Na Beki wa United raia wa Argentina Marcos Rojo, 29, yuko tayari kupigania uhamisho wa mwezi Januari mbali na klabu hiyo iwapo atahitajika kufanya hivyo baada ya uhamisho wake wa kuelekea Everton kugonga mwamba. (Ole - in Spanish)
Mabingwa wa Itali Juventus wanafikiria kumnunua beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27.
Inter Milan pia wana hamu ya kumsajili Alderweireld. (Mail)
Mabingwa wa Uhispania Barcelona walitaka kumsaini winga wa Itali mwenye umri wa miaka 25 Federico Bernardeschi kutoka Juventus katika dirisha la uhamisho la msimu huu (Mundo Deportivo - in Spanish)
TETESI YA IJUMAA
Mshambulizi wa Juventus, Paulo Dybala
Tottenham itapewa nafasi nyingine ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 25 mbaye thamani yake inakadiriwa kuwa £65m-dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa tena mwezi Januari mwaka. (Star)
Atletico Madrid wanapigiwa upatu wa kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, Januari mwaka ujao. (Express)
Juventus inamtaka Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, na wachezaji wengine wa klabu hiyo Eric Bailly, 25, na Nemanja Matic, 31, huenda ikiweka dau la kuwanunua msimu ujao. (Gazzetta Dello Sport, via Team Talk)
Kipa wa Manchester United, David de Gea
Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 27, amekataa kuthibitisha au kukana tetesi kuhusu uhamisho wake kwenda Manchester United au Arsenal mwezi Januari mwakani huku kandarasi yake ikitarajiwa kikamilika msimu ujao. (RTBF, via Mirror)
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ameridhishwa na utendajikazi wa Gareth Bale,30, na anaamini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales, akishirikiana vizuri na Eden Hazard, watakua kiungo muhimu katika mradi mpya wa Real Madrid. (ESPN)
Gareth Bale
Bale amesema anatarajia "misuko suko mingi "kabla ya "uamuzi" kuhusu hatma yake Real Madrid. (Sky Sports)
Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho alikataa kumsaini Virgil van Dijk mwezi Januari 2018, kabla ya mchezaji huyo kujiunga na Liverpool. (Independent, via Liverpool Echo)
Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyomnyatia vinga wa miaka 20 wa Villarreal na Nigeria Samuel Chukwueze. (Goal)
Kiungo safu ya ulinzi ya Liverpool, Virgil van Dijk
Inter Milan ilimuulizia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Mjerumani Mario Gotze mwezi Agosti na huenda ikamnunua mshezaji huyo wa miaka 27 Januari mwakani. (La Gazzetta dello Sport)
Juhudi za Tottenham kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, ziligonga mwamba kutokana "ugumu" wa mfumo wa kuwasilisha ofa, amesema rais wa Sporting Frederico Varandas. Spurs ilikua tayari kulipa £40m kabla ya mkataba kufikiwa na baadae kuongeza £18m ikiwa wangelishinda Ligi ya Premia na Champions League. (Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandes
Beki wa Derby Krystian Bielik, 21, anasema AC Milan ilitaka kumsajili kabla aondoke Arsenal kwenda Rams. (Derby Telegraph)
Tetesi Bora Alhamisi
Barcelona ingelimsaini mshambuliaji wa Tottenham Lucas Moura, 27, msimu huu lakini ilishindwa kufikia bei yake ya £45m. (Mundo Deportivo)
Juventus itawauza mshambuliaji Mario Mandzukic, 33, na kiungo wa kati Emre Can, 25, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari. (Goal)
Mshambulizi wa Tottenham Lucas Moura
Atletico Madrid bado inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, na wako tayari kuweka dau kubwa mwezi Januari. (AS - Spanish)
Beki wa Liverpool Dejan Lovren, 30, amesema anatathmini uwezekano wa kuhamia AC Milan na Roma msimu huu wa joto. (Sportske Novosti via Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, alilia machozi alipoambiwa kuwa hawezi kujiunga tena na klabu yake ya zamani Barcelona. (El Chiringuito radio via Esporte - Portuguese)
Neymar
Mshambulizi wa Barcelona Luis Suarez, 32, amesema Neymar alikua amefanya kila awezalo kuondoka Paris St-Germain. (Fox Sports Radio via Barca Blaugranes)
Vilabu vya Real Sociedad na Athletic Bilbao nchini Uhispani vinajiandaa kumnyakua beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 30, ikiwa mchezaji huyo atapatikana. (Express)
Callum Hudson-Odoi, 18, amabye ni mshambuliaji wa Chelsea yuko tayari kujitolea kwa mustakabali wake wa muda mrefu na klabu hiyo. (Football.london)
Kiungo wa safu ya mashambulizi ya Chelsea Callum Hudson-Odoi
Ndugu yake kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa miaka 26 atatumia muda wake mwingi Old Trafford kujiimarisha bada ya jaribio lake la kuhama klabu hiyo msimu huu kugonga mwamba. (El Chiringuito via Metro)
Beki wa Liverpool Dejan Lovren, 30, amesema anatathmini uwezekano wa kuhamia AC Milan na Roma msimu huu wa joto. (Sportske Novosti via Liverpool Echo)
Post a Comment