Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha wa timu ya Yanga kwa sasa ameweka msisitizo wa timu yake kufika katika rekodi ambayo iliwekwa na wapinzani wao wa jadi, Simba, msimu uliopita kwa kucheza hatua ya makundi.
“Tunataka kufika katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hilo ndiyo lengo letu ambalo tumejiweka wachezaji kwa sasa.
“Tunajua itakuwa mechi ngumu tutakapopambana na Zesco lakini tutapambana kuona tunashinda na kutinga kwenye makundi kama kila moja anavyotamani hapa,” alisema Tshishimbi.
Yanga inakutana na Zesco baada ya kuitupa nje Township Rollers katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1.
Post a Comment