Mwandishi wetu, LISBON, URENO

KLABU ya Sporting Lisbon ya Ligi Kuu Ureno,  imeripotiwa kuanza mazungumzo na KRC Genk,  kwa ajili ya kupata saini ya nahodha wa timu ya Taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’,  Mbwana Samatta.

Sporting Lisbon ambayo pia inafahamika kama Sporting CP  ndiyo klabu iliyomwibua na  kumkuza staa wa  Juventus  na timu ya Taifa ya Ureno, Christiano Ronaldo kabla ya kuivutiwa Manchester iliyomsajili mwaka 2003 kwa pauni milioni 19.

Samatta mwenye umri wa miaka 27, alikaribia kutua Ligi Kuu ya England,  baada ya kufukuziwa na klabu za huko zikiwemo Burnley, Watford, Everton, WestHam na Cardif  iliyoshuka daraja kuonyesha nia ya kumsajili, lakini dau ya Euro Milini 12 lililowekwa na Genk lilionekana kuzikwamisha hadi pale dirisha la usajili nchini humo lilipofungwa Agosti 8, mwaka huu.

Hata hivyo, Samatta anaweza kukamilisha uhamisho wa kwenda Ureno katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili barani Ulaya linalofungwa leo.

Mshambulaji huyo alikuwa na kiwango bora msimu uliopita, akifunga mabao 23 na kuisadia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Ubelgiji na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu  huu.

Mabao hayo yalimfanya Samatta kumaliza nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji , mabao mawili nyuma ya Hamdi Harbaoui wa Zulte Waregem aliibuka kinara baada ya kufunga mabao 25.

Ubora wake huo ulimwezesha pia kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaokipiga Ligi ya nchini Ubelgiji msimu uliopita, tuzo hiyo ni maarufu kwa jina la Ebony Shoe Award.

Samatta ameuanza msimu  huu kwa kishindo,  baada ya kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya wafungaji wa ligi hiyo, akiwa tayari amefunga mabao matano kupitia michezo mitano aliyoshuka dimbani na Genk.

Mtandao wa TUTTOmercato Web.com  wa nchini Ureno, umeripoti kuwa,  Samatta hana muda mrefu kwenye kikosi cha Genk,  baada ya Sporting Lisbon kuanza mazungumzo na timu yake hiyo,  ili kuangalia uwezekano wa kumnasa.

Mbali na Lisbon, mtandao huo umedai kuwa klabu ya St Etienne ya Ufaransa nayo imejitosa  kumfukuzia staa huyo wa zamani wa Simba ya hapa nchini na TP ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Hata hivyo, timu zote hizo zitahitaji kuwa na ushawishi mkubwa kwa Samatta ili aondoke Genk na kujiunga nazo , kwani  hazijafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Katika michuano hiyo, Genk imepangwa kundi E pamoja na mabingwa watetezi, Liverpool ya England, Napoli ya Italia na Salzburg ya Austria.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.