Paris, Ufaransa /AFP/. Christiano Ronaldo, ambaye ametwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mara tano, atapata dola milioni 139 milioni za Kimarekani (sawa na takriban Sh320 bilioni za Kitanzania) katika mkataba wake na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike.
Hiyo imebainika katika nyaraka za Football Leaks zilizokaririwa na jarida la michezo la Der Spiegel lililotoka jana Ijumaa.
Mkataba wake mpya, ambao utaisha mwaka 2016, pia unajumuisha bonasi ya dola 4 milioni kwa kushinda tuzo binafsi, kwa mujibu wa mkataba wa awali.
Ronaldo, ambaye alijiunga na Juventus mwaka 2018, baada ya kuichezea Real Madrid na Manchester United katika kipindi kilichompatia vikombe kadhaa, amekuwa na mkataba na kampuni kubwa ya nguo ya Marekani tangu mwaka 2004 "ambao ulimhakikishia ada ya euro 3.65 milioni".
"Kwa kadri Ronaldo atanavyochezea klabu ya Daraja A, anatakiwa alipwe euro 16.2 milioni (sawa na Sh411 bilioni za Kitanzania) kila mwaka," jarida hilo la Ujermani limesema.
Nike ilijibu taarifa ya jarida hilo kw akusema: "Hatuzungumzii mikataba ya wanamichezo."
Mchezaji wa Ujerumani anayepata malipo makubwa katika orodha hiyo ni kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil, ambaye anapata euro 1.2 milion kwa mwaka kutoka kampuni pinzani ya Adidas.
Kiwango hicho cha Ozil kilishuka kwa euro 800,000 baada ya kutangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa mwaka 2018.
Post a Comment