Miamba hiyo ya Hispania, Los Blancos walikuwa na mpango wa kunasa saini ya kiungo huyo ambaye Man United walidai watakuwa tayari kumuuza kwa ada ya Pauni 150 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND. IMEFICHUKA kwamba Paul Pogba amebaki Manchester United kwa sabbu tu ya wadhamini kampuni ya Adidas.
Kiungo huyo ametajwa karibu muda wote wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kwamba anataka kuondoka Old Trafford kwenda kukipiga huko Real Madrid.
Miamba hiyo ya Hispania, Los Blancos walikuwa na mpango wa kunasa saini ya kiungo huyo ambaye Man United walidai watakuwa tayari kumuuza kwa ada ya Pauni 150 milioni.
Lakini, Pogba amebaki kuwa mchezaji wa Man United na taarifa zilizopatikana ni kwamba kampuni ya Adidas ndio sababu kubwa ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuendelea kubaki huko Old Trafford.
Kampuni hiyo ya Kijerumani ndio kwanza ipo kwenye mwaka wa tatu kati ya miaka 10 ya mkataba wao na mchezaji huyo, wenye thamani ya Pauni 31 milioni. Lakinni, pia ndio wanaotengeneza jezi za miamba hiyo ya Old Trafford kwenye dili lao lenye thamani ya Pauni 750 milioni ambalo liko hadi hadi 2024.
Kumekuwa na maelezo kwamba Adidas imehakikisha kwamba Pogba anaendelea kubaki kwenye kikosi cha Man United walau kwa mwaka mmoja zaidi. Chanzo cha ripoti kilibainisha: “Walikuwa kama wasuluhishi kati ya mchezaji, wakala wake na klabu.
“Adidas walikuwa watu muhimu katika kuziweka kawa pande zote kuondoa tofauti ambazo ziliibuka katika kipindi cha mchakato huo.”
Adidas pia ndio wanatengeneza jezi wa Real Madrid, lakini Pogba ni mmoja tu wa mastaa kibao wanaomilikiwa na kampuni hiyo, ambapo wengine baadhi ni Gareth Bale na Karim Benzema.
Mechi 3 zijazo za Man United
Sept 14 vs Leicester City - nyumbani
Sept 19 vs Astana - nyumbani
Sept 22 vs West Ham - ugenini

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.