kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kuu, imefanya kikao chake septemba 2, 2019 kupitia matukio mbalimbali ya ligi kuu ya vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi wa kumuadhibu kocha wa Yanga pamoja na klabu yake.
Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za ligi kuu ya vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa bodi ya ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting.
Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 41(13) ya ligi kuu kuhusu udhibiti kwa makocha huku waajiri wake ambao ni klabu ya Yanga wamepewa onyo kwa kushindwa kuhakikisha kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima.
Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14(3) ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.
Pia Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kudaiwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na kanuni ya 14(2m) ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.
Post a Comment