Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubelgiji huenda Mbappe akawa mrithi wa Mbwana Samatta ambaye anatazamiwa kuondoka KRC Genk kipindi cha usajili cha Januari, mwakani.
NYOTA wa timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’, Kelvin Pius John ‘Mbappe’ yuko mbioni kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anayoichezea nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubelgiji huenda Mbappe akawa mrithi wa Mbwana Samatta ambaye anatazamiwa kuondoka KRC Genk kipindi cha usajili cha Januari, mwakani.
Kutokana na kanuni za kisheria za kuingia na kukaa Ulaya hasa kutokana na udogo wa umri wake, itambidi kinda huyo wa Kitanzania aingie Ubelgiji kama mwanafunzi ambaye atakuwa akicheza soka kwenye kituo cha chama hilo.
Mbappe huyo wa Tanzania, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa nchini akiwa na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, aliwahi kufanya majaribio ya kujiunga na HB Køge ya Denmark.
Kinda huyo pia aliwahi kufanya majaribio na kufuzu nchini Afrika Kusini kwenye klabu ya Ajax Cape Town huku akitazamwa na kipa wa zamani wa Manchester United, Edwin van der Sar.
Edwin van der Sar alienda Afrika Kusini kutokana na uhusiano uliopo baina ya Ajax ya nchini kwao Uholanzi ambayo alikuwa akiifanyia kazi na timu hiyo yenye maskani yake Cape Town.
Dili la kinda huyo wa Kitanzania, linatarajiwa kutangazwa rasmi ndani ya mwezi huu baada ya kulitumikia Taifa katika Mashindano ya Cecafa U20 yatakayofanyika nchini Uganda.
Mbappe ataungana na Faissal Boujemaoui wa
Morocco ambaye alikuwepo nchini hapa akilitumikia Taifa lake kipindi cha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Post a Comment