Klabu ya Celtic ya Uskochi inaweza kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya Tottenham na Kenya Victor Wanyama, 28, mwezi Januari, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Neil Lennon. Wanyama aliwika na Celtic kabla ya kutimkia England, na sasa kocha wa Tottenham ameshaeleza kuwa hana haja naye. (Team Talk)
Winga wa Chelsea na Brazil Willian anataka kusalia kwenye uga wa Stamford Bridge, lakini klabu hiyo hata hivyo bado haijampatia nyota huyo mwenye miaka 32 mkataba mpya. (Express)
Beki wa Ajax na Uholanzi Joel Veltman, 27, amebainisha kuwa alitaka kujiunga na klabu ya West Ham United ya England katika dirisha la usajili lililopita lakini mabingwa hao wa Uholanzi hawakumruhusu kuindoka. (NOS - in Dutch)
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ataendelea na mipango ya kusajili wachezaji kutoka Uingereza msimu ujao wa dirisha la usajili la majira ya joto.
Wachezaji ambao wapo kwenye rada ya Solskjaer ni mshambuliaji kinda wa England na klabu ya Borussia Dortmund Sancho, 19, na kiungo wa Leicester City na England James Maddison 22. (ESPN)
Miamba ya soka ya Italia, vilabu vya AC Milan, Inter Milan, Juventus na Borussia Dortmund zote zipo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United Nemanja Matic, 31, pale mkataba wa mchezaji huyo wa kimataiifa wa Serbia utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu. (Calcio Mercato - in Italian)
Liverpool walipanga kumsajili mlinzi wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly iwapo mipango yao ya kumsajili beki kisiki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ingegonga mwamba mwezi Januari 2018. (Goal)
Bournemouth wanajiandaa kumpatia Ryan Fraser,25, mkataba mpya wa mshahara wa thamani ya pauni 100,000 kwa wiki. Tayari vilabu vya Arsenal, Everton, Chelsea NA Wolves vyote vinamnyemelea winga huyo raia wa Uskochi. (90min.com)
Mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson
Bournemouth pia wanaweza kumpoteza mshambuliaji wao Callum Wilson, 27, anayenyemelewa na Manchester United.(ESPN)
Beki wa klabu ya Watford na Ubelgiji Christian Kabasele, 28, amebainisha kuwa anakaribia kusaini mkatabampa na klabu yake. (Sport Witness)
Everton, Southampton, Bournemouth, Sheffield United, Bristol City, Barnsley na Sunderland wote wanamfuatilia kwa makini winga kinda wa klabu ya Motherwell ya Uskochi James Scott, 19. (Team Talk)
Tetesi za Jumatatu
Real Madrid na Barcelona zinatarajiwa kushindana pakubwa kuwania kumvutia meneja Jurgen Klopp na mlinzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Liverpool. (AS, kupitia Star)
Manchester United imejitolea kumfanya kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, kuwa mcheza soka anayelipwa pakubwa katika ligi kuu ya England katika kumshawishi kusaini mkataba mpya wa muda mrefu (Times)
Christian Eriksen anapuuzia mkataba mpya anaopendekezewa na Tottenham wakati wakala wa mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 27akishughulikia uhamisho kwenda Real Madrid msimu ujao wa joto. (Marca, kupitia Express)
Mchezaji wa kiungo cha mbele Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, na kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid, baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chelsea mwenye miaka 28, kuhusishwa na uhamisho kwenda Uhispania. (Sun)
Eden Hazard, na kipa Thibaut Courtois, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid
Huenda Real Madrid ikamkabidhi mchezaji wa kiungo cha kati Toni Kroos, kwa Manchester United ili kwa upande wake ijipatie mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26 Paul Pogba. (FourFourTwo)
Arsenal inakaribia kufanikiwa kumsajili kijana wa Sunderland Logan Pye baada ya mchezaji huyo wa miaka 15 kuhusishwa ma uhamisho kwenda katika ligi kuu ya England wakati wa msimu wa joto. (Sun)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United, Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, yuko kwenye rada ya Juventus huku kukiwadia kinachowezekana kuwa ni mageuzi ya Januari. (Mirror)
Baada ya kuwasajili wachezaji 12 katika uhamisho wa msimu wa joto, mipango imeidhinishwa kwa Aston Villa kushughulika kwa mara nyingine katika dirisha la Januari. (Birmingham Mail)
Manchester United ilituma mawakala kumchunguza mshambuliaji wa Kosovo, Vedat Muriqi, mwenye umri wa miaka 25, wakati alipofunga dhidi ya timu ya England huko Wembley Jumanne usiku. (Express)
Meneja wa Arsenal, Unai Emery amefichua kwamba alikuwa na Javi Gracia wakati Watford ilipomfuta kazi. (Metro)
Bingwa wa Manchester United Gary Neville amesema anaweza 'kukimbia maili moja' iwapo atapewa kazi ya U meneja Old Trafford. (Manchester Evening News)
Post a Comment