Na Shabani Rapwi
Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars”,
Ettiene Ndayiragije amewaongeza wachezaji watatu katika kikosi chake, wachezaji hao ni Oscar Masai wa Azam FC, Haruna Shamte kutoka Lipuli FC na Golikipa wa Lipuli FC, Mohamed Yusufu.
Wachezaji hao wameitwa katika kikosi hiko kuziba nafasi ya wachezaji watatu, Aishi Manula , David Mwantika na Ibrahim Ajib ambao ni majeruhi.
Kikosi cha Taifa Stars kipo kambini kujiandaa na mchezo wapili wa kufuzu CHAN dhidi ya Kenya utakaopigwa Agosti 04, 2019 nchini Kenya baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya 0-0 uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Post a Comment