Mshambuliaji wa zamani wa Simba,Laudit Mavugo amejiunga na Difaa El Jadida ya Morocco ambayo pia anaichezea nyota wa Kimataifa wa Tanzania, Saimon Msuva.

NYOTA wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Burundi,   Laudit  Mavugo amejiunga na  Difaa El Jadida ya Morocco anayoichezea Saimon Msuva na Nickson Kibabage kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Mavugo amesaini mkataba huo jana Ijumaa ambapo msimu uliopota akiwa na Napsa Stars  ya Zambia aliibuka mfungaji bora wa ligi hiyo, akiwa na mabao 10.
Baada ya kujiunga na Difaa,  Mavugo alisema amefurahi kupata nafasi ya kujiunga na  timu hiyo huku akiamini kwamba atakuwa na maelewano mazuri na Msuva kama wakiwa wanacheza pamoja mara kwa mara.
"Msuva  ana mbio ambazo zinaweza kunifanya kufunga zaidi,  napenda anavyocheza sidhani kama nahitaji muda wa kuzoeana naye,  naweza kuhitaji muda kwa wachezaji wengine, " alisema Mshambuliaji.
Mavugo alisema kucheza kwake soka la Bongo kumemfanya kuwa bora na ndio maana msimu uliopita aliibuka kuwa mfungaji bora.
"Kuna mengi ambayo nilijifunza Tanzania licha ya kupitia changamoto kadhaa niliwajibika kukabiliana nazo kwa sababu mbali ya kuwa mpira ni kazi lakini pia sehemu ya maisha yangu, " alisema.
MSUVA AMPA MZUKA
Msuva  ambaye huu utakuwa msimu wake wa tatu Morocco,  alisema kama mwenyeji anawajibika kutoa ushirikiano kwa Mavugo ili kuzoea kwa haraka soka la nchi hiyo.
"Niliipata nilivyojiunga Difaa kwa sababu hapakuwa na mtu wa kuongea naye mara kwa mara. Amekuja Mavugo na Kibabage ambao nafanya nao mawasiliano kwa wepesi.
"Naamini Mavugo ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kuongeza nguvu kwenye timu yetu, " alisema Msuva ambaye alijiunga na Difaa akitokea Yanga, 2017.
Ndani ya misimu miwili ambayo Msuva ameichezea Difaa,  ameifungia klabu hiyo jumla ya mabao 24, yakiwemo 13 ya msimu uliopota kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama Batola Pro.
Wakati huo huo,  Msuva alisema atajiunga na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' nchini Burundi ambako watacheza mchezo wa kwanza,  Septemba  4 wa kuwania nafasi ya kwenda kombe la dunia nchini Qatar 2022 ambapo ataondoka Morocco leo Jumapili na kufika Burundi kesho Jumatatu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.