Aliyekuwa mchezaji Yanga, Mrundi, Amis Tambwe, amesema kuwa kitendo cha klabu hiyo kufanya mabadiliko ya nafasi ya msemaji haina maana ya kuwa itachangia kuleta hamasa ya mashabiki kwenda kwa wingi uwanjani.

Tambwe ambaye hivi sasa hayupo Yanga na ikielezwa amejiunga na Fanja FC ya Oman, anaamini kuwa suala la timu kufanya vema ndilo linaloleta matokeo uwanjani.

Amesema kipindi ambacho Yanga ilikuwa chini ya Hans van der Pluijm ilikuwa inaleta mashabiki wangi dimbani na wakati huo walipokuwa wakikutana na timu dhaifu walikuwa wanazifunga mabao saba mpaka nane.

"Suala la kubadilisha msemaji halina maana yoyote kama timu haifanyi vema.

"Nadhani matokeo ndiyo huleta mashabiki kwa wingi uwanjani, Yanga wanapaswa kufanya vizuri ili kupata mashabiki kwa wingi."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.