Sura Mpya Kibao Kuivaa Mtibwa Taifa Kesho
KESHO Simba itatupa kete yake ya pili kucheza na Mtibwa Sugar lakini safari hii sura nyingi mpya zitaonekana kwenye kikosi cha kwanza.
Kwa mujibu wa mazoezi ya jana, inaonekana kwamba Aussems atapangua kikosi kitakachoivaa Mtibwa ili kuimarisha ufanisi wa Simba na kuonyesha dhana ya kikosi kipana. Jana alichezesha vikosi viwili mazoezini.
Kikosi cha kwanza kilikuwa kinaundwa na Aishi Manula ambaye ni mlinda mlango na upande wa mabeki ilikuwa ni Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Shomari Kapombe, Fraga Vieira, kwa upande wa viungo ni Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Fraga Vieira, Clatous Chama, Shiboub na mshambuliaji alikuwa ni Miraji Athuman.
Kwa upande wa kikosi cha pili kiliundwa na Beno Kakolanya ambaye alikuwa ni mlinda mlango kwa upande wa mabeki Pascal Wawa, Haruna Shamte, Kennedy Juma na Gadiel Michael upande wa viungo wakiwa ni Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Francis Kahata na kwa upande wa washambuliaji akiwa Deo Kanda na Rashid Juma.
Mwishoni kabisa alimfanyia mabadiliko Jonas Mkude na Fraga Vieira, Tshabalala alichukua nafasi ya Gadiel.
Post a Comment