Bigirimana alisema kutokana na maumivu hayo ya paja ameshindwa kuyaelewa na kuna wakati anajiona yuko vizuri lakini baadaye mambo hubadilika na kuwa mabaya zaidi.
YANGA inaendelea na maandalizi yake kujiwinda na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ya Zambia lakini ukiacha Patrick Sibomana ambaye yupo na timu ya taifa yake kuna mshambuliaji mmoja amejiondoa mapema katika kikosi hicho.
Mshambuliaji Issa Bigirimana hayupo katika kikosi cha Yanga sasa akibaki jijini Dar es Salaam ameliambia Mwanaspoti hataweza kuingia kambini kufanya maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Zesco.
Bigirimana raia wa Burundi jana Jumapili alikuwepo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kama shabiki akiliangalia taifa lake la Burundi akisema maumivu ya paja ndiyo yanayomtesa kwa sasa.
Bigirimana alisema kutokana na maumivu hayo ya paja ameshindwa kuyaelewa na kuna wakati anajiona yuko vizuri lakini baadaye mambo hubadilika na kuwa mabaya zaidi.
“Sijaenda na timu nipo hapa Dar es Salaam kama unavyoniona naumwa nyama ndugu yangu,” alisema Bigirimana.
“Kwakweli nimekuwa sielewi haya maumivu yanatokea wapi, kwa sababu yananinyima raha. Kuna wakati najiona niko salama kabisa lakini baada ya muda yanarudi. Nikitaka kuanza mazoezi hali inarudi na kuwa mbaya zaidi,” alisema kwa masikitiko.
Aidha Bigirimana alisema kwasasa yuko katika mchakato wa kubadilishiwa daktari kwa ajili ya maumivu hayo ambayo tangu amefika hajacheza mechi yoyote ya kimashindano.
“Nimeambiwa kuna daktari mwingine nitapelekwa ili naye akaniangalie ndiyo nasubiri kuona mambo yatakuwaj.”
Akiwa kambini Morogoro katika maandalizi ya msimu mpya Bigirimana alikuwa moto akifunga mabao makali lakini hali ikabadilika alivyotua jijini Dar es Salaam.
Yanga ya Kocha Mwinyi Zahera iko kwenye changamoto ya washambuliaji wake kutotumia nafasi katika mechi zake.
Inaamika kama straika huyo angekuwa fiti mambo yangebadilika na labda Yanga isingekuwa na shida katika upachikaji wa mabao.
Mara nyingi makocha huwataka wachezaji wao hata wakiwa majeruhi kusafiri au kwenda kutazama mazoezi lakini kwa Bigirimana imeshindikana kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.
Post a Comment