Farid ambaye alijiunga na CD Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza Hispania maarufu kama Segunda, amefichua hilo wakati akiwa kambini kabla ya mchezo wa jana dhidi wa Burundi wa kuwania kufuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Qatar, 2022.
KIWANGO alichoonyesha winga wa Kitanzania, Farid Mussa kwenye mchezo wa makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Kenya kimeziweka njia moja klabu kadhaa barani Ulaya kusubiri huduma yake ifikapo Januari, mwakani.
Farid ambaye alijiunga na CD Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza Hispania maarufu kama Segunda, amefichua hilo wakati akiwa kambini kabla ya mchezo wa jana dhidi wa Burundi wa kuwania kufuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Qatar, 2022.
Winga huyo alisema kuna zaidi ya timu tatu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili, hivyo Januari anaweza kuachana na chama lake la CD Tenerife na kujiunga na miongoni mwa timu hizo.
“Naweza kuondoka Januari CD Tenerife, ni zaidi ya asilimia 80 kwa sababu kuna timu ambazo zilivutiwa na uwezo wangu kipindi cha Afcon, nadhani ni muda sahihi kwangu kwenda kujaribu kwingine,” alisema mchezaji huyo katika mahojiano na Mwanaspoti.
“Nina shauku ya kucheza kwa mafanikio, nilichojifunza hapa naweza kukitumia huko ambako naweza kwenda. Zipo timu za Hispania na nyingine za mataifa mengine ya hukohuko Ulaya.”
Tangu ajiunge na CD Tenerife, Farid mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akitumika kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo ambacho kinashiriki Ligi Daraja la Tatu nchini humo ambayo inafahamika zaidi kama Tercera.
Mchezaji huyo alisema klabu hizo ambazo zinataka kumsajili zilivutiwa naye na uwezo ambao aliuonyesha kwenye mchezo wa Afcon, Juni 27 ambapo Taifa Stars ilipoteza kwa mabao 3-2 mbele ya Kenya.
Katika mchezo huo, Farid alionyesha kiwango cha juu kwa akishiriki kusababisha bao la kwanza ambapo alipiga pasi akiwa katikati ya uwanja iliyomfikia Mbwana Samatta ambaye alipiga shuti lililochezwa na kipa wa Kenya kabla ya Saimon Msuva kumalizia kirahisi.
Kabla ya kutimkia Hispania, Farid alikuwa akikipiga Azam FC ya jijini Dar es Salaam na aliondoka nchini mwaka 2016.
Post a Comment