Neymar

Barcelona wamesitisha jaribio lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymarkutoka Paris Saint-Germain hadi msimu ujao. (ESPN)

Mazungumzo kati ya vilabu hivyo yalivunjika baada ya PSG kulegeza masharti yao licha ya Neymar kujitolea kulipa £17.7m kufikia makubaliano ya usajili wake. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao alipokelewa na mashabiki 25,000 alipowasili Istanbul siku ya jumapili kabla ya pendekezo la kujiunga Galatasaray kutoka Monaco. (Mirror)

Roma wanamatumaini ya kusaini kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ,30. (Sky Italy - in Italian)

Henrikh Mkhitaryan

Beki wa zamani wa Liverpool Martin Skrtel amevunja mkataba wake na Atalanta inayoshiriki Ligi ya Serie ya Italia wiki kadhaa baada ya kujiunga na klabu hiyo. (Mail)

Mshambuliaji wa Frankfurt mwenye umri wa miaka 25 Mcroatia Ante Rebic anajiandaa kujiunga na AC Milan, huku mshambuliaji Andre Silva, 23 Mrenoakitarajiwa kujiunga na klabu hiyo. (Goal)

Kipa wa Paris St-Germain Alphonso Areola, 26, anatarajiwa kumilisha uhamisho wake kwenda Real Madrid siku ya mwisho katika mkataba ambao utamwezesha kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, kujiunga na klabu hiyo. (Mirror)

PSG wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 26, kwa mkopo kutoka Inter Milan. (RMC Sport - in French)

Mlinzi wa Bayern Munich Mjerumani Jerome Boateng, 30, anakaribia kujiunga na mabingwa wa Italia uventus. (Bild, in German)

Juventus hawajakatiza matumaini ya kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona'wa miaka 31 Mcroatia Ivan Rakitic - na huenda wakatoa ofa ya kumuachilia mchezaji wa kiungo cha kati Mjerumani Emre Can, 25, kama sehemu ya kufikia mkataba wa kumsajili Ivan Rakitic. (Sport - in Spanish)

Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti anasema kuwa yuko tayari kumsaini mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 37, kutoka LA Galaxy. (Sun)

Borussia Dortmund wanapigiwa upatu kumsajili kipa wa Liverpool wa miaka 18 Bobby Duncan ikiwa klabu hiyoo ya Ligi Kuu ya Uingereza ataamua kukomesha mkataba wake . (Mirror)

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.