Aliyekuwa kocha wa timu ya kandanda nchini Tanzania Emmanuel Amunike amelishtaki shirikisho la soka la Tanzania TFF kwa shirikisho la mchezo huo duniani FiFa akilalamikia kutolipwa haki yake.
Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania lililonukuu mtandao wa Complete Sport.com na Punching.com , Kocha huyo raia wa Nigeria ameamua kuwasilisha malalamishi hayo kwa Fifa ili kutafuta haki yake.
Amunike alitimuliwa na shirikisho la soka la Tanzania baada ya tanzania kupata matokeo duni katika kombe la mataifa ya Afrika .
''Nimewasiliana na Fifa juu ya hilo jambo . Sio Swala la kupiga kelele , lakini nina imani watalitazama na kuamua iwapo ni sahihi mtu kutolipwa baada ya kufanya kazi'', Amunike alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema.
Kocha huyo ambaye mkataba wake ulivunjwa mwezi Julai mwaka huu amerejea Uhispania ambako makazi yake ya kudumu yapo.
Kwa mujibu wa Mwananchi , TFF waliafikia uamuzi huo wa kuvunja mkataba na kocha mchezaji huyo wa zamani wa Nigeria baada ya taifa Stars kuandikisha matokeo mabaya katika fainali ya Afcon 2019 zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19.
Katika fainali hizo taifa Stars ilishika mkia kwenye kundi C lililokuwa na Senegal, Kenya, na Algeria baada ya kupoteza mechi zote ta
Kushindwa kwao na majirani zao kenya ndio kulikohuzunisha wengi kwa kuwa walipoteza uongozi waliokuwa nao wa 2-0 kufikia kipindi cha mapumziko.
Na kufuatia matokeo hayo Amunike alisea kwamba timu hiyo ilihitaji uzoefu wa mashindano makubwa na kwamba wachezaji walihitaji kushiriki katika ligi zenye ushindani mkubwa ili kuweza kuimarika.
Kocha huyo ambaye mwenye umri wa miaka 47 ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka klabu ya Sudan ya A; Khartoum mnamo mwezi Machi aliandikisha mkataba wa miaka miwili na taifa hilo la Afrika mashariki akichukua nafasi yake Saulm Mayanga.
Amunike alishinda kombe la Afrika akiichezea Super Eagles ya Nigeria 1994 na mshindi wa dhahabu ya Olimpiki miaka miwili baadaye.
Katika kipindi chake cha mchezo aliichezea, SC Zamalek, Sporting \lisbon, na Barcelona ijapokuwa majeraha yalimzuia kuafikia ndoto yake mjini Catalonia.
Winga huyo wa zamani alianza ukufunzi na timu ya nigeria isiozidi wachezaji wa miaka 17 2014 na kushinda kombe la dunia la kinda hao mwaka mmoja baadaye.
Post a Comment