LONDON, ENGLAND. ARSENAL wanajiamini kwamba straika wao Pierre-Emerick Aubameyang atasaini dili jipya na kuendelea kukipiga kwenye kikosi chao kwa muda mrefu.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon amekuwa kwenye kiwango bora huko Arsenal tangu alipojiunga akitokea Borussia Dortmund kwenye dirisha la Januari 2018 - akifunga mabao 44 katika mechi 69 alizoitumikia klabu hiyo ya London.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 30 ameshafunga mabao matatu katika mechi nne za Ligi Kuu England alizochezea Arsenal msimu huu, huku mabao hayo likiwamo la kusawazisha dhidi ya mahasimu wao Tottenham Hotspur kwenye London derby wikiendi iliyopita.
Dili la sasa la Aubameyang huko Emirates litafika tamati Juni 2021, lakini Manchester United kuna wakati walitajwa kuwa na mpango wa kunasa saini yake.
Hata hivyo, football.london, inaripoti kwamba kikosi hicho kinachonolewa na kocha Unai Emery kina imani kubwa kwamba mshambuliaji wao atasaini mkataba mrefu wa kuendelea kubaki kwenye kikosi chao.
Aubameyang alifunga mabao 141 katika mechi 213 alizocheza Dortmund kabla ya kutua zake Arsenal kwa ada ya Pauni 56 milioni kipindi hicho timu ilipokuwa chini ya kocha Arsene Wenger.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.