Kwa mara ya kwanza mchezaji wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez amewaambia waandishi wa habari kuwa, kamwe hatajutia uamuzi wake wa kujiunga na klabu ya Manchester United mwezi Januari mwaka 2018, japo anakiri kuwa hakupata muda mwingi wa kucheza katika klabu hiyo ili ayafikie mafanikio.

Sanchez ambaye alikuwa mchezaji anayelipwa zaidi Manchester United kwa mshahara wa pauni laki nne kwa wiki moja, alicheza jumla ya mechi 45 na kufunga magoli matano tu, tofauti na magoli 80 aliyofunga katika mechi 166 akiwa na Arsenal.

Kwa sasa Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona amejiunga na klabu ya InterMilan ya Italia kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.