September 2019

Klabu ya Celtic ya Uskochi inaweza kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya Tottenham na Kenya Victor Wanyama, 28, mwezi Januari, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Neil Lennon. Wanyama aliwika na Celtic kabla ya kutimkia England, na sasa kocha wa Tottenham ameshaeleza kuwa hana haja naye. (Team Talk)

Winga wa Chelsea na Brazil Willian anataka kusalia kwenye uga wa Stamford Bridge, lakini klabu hiyo hata hivyo bado haijampatia nyota huyo mwenye miaka 32 mkataba mpya. (Express)

Beki wa Ajax na Uholanzi Joel Veltman, 27, amebainisha kuwa alitaka kujiunga na klabu ya West Ham United ya England katika dirisha la usajili lililopita lakini mabingwa hao wa Uholanzi hawakumruhusu kuindoka. (NOS - in Dutch)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ataendelea na mipango ya kusajili wachezaji kutoka Uingereza msimu ujao wa dirisha la usajili la majira ya joto.

Wachezaji ambao wapo kwenye rada ya Solskjaer ni mshambuliaji kinda wa England na klabu ya Borussia Dortmund Sancho, 19, na kiungo wa Leicester City na England James Maddison 22. (ESPN)

Miamba ya soka ya Italia, vilabu vya AC Milan, Inter Milan, Juventus na Borussia Dortmund zote zipo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United Nemanja Matic, 31, pale mkataba wa mchezaji huyo wa kimataiifa wa Serbia utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu. (Calcio Mercato - in Italian)

Liverpool walipanga kumsajili mlinzi wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly iwapo mipango yao ya kumsajili beki kisiki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ingegonga mwamba mwezi Januari 2018. (Goal)

Bournemouth wanajiandaa kumpatia Ryan Fraser,25, mkataba mpya wa mshahara wa thamani ya pauni 100,000 kwa wiki. Tayari vilabu vya Arsenal, Everton, Chelsea NA Wolves vyote vinamnyemelea winga huyo raia wa Uskochi. (90min.com)

Mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson

Bournemouth pia wanaweza kumpoteza mshambuliaji wao Callum Wilson, 27, anayenyemelewa na Manchester United.(ESPN)

Beki wa klabu ya Watford na Ubelgiji Christian Kabasele, 28, amebainisha kuwa anakaribia kusaini mkatabampa na klabu yake. (Sport Witness)

Everton, Southampton, Bournemouth, Sheffield United, Bristol City, Barnsley na Sunderland wote wanamfuatilia kwa makini winga kinda wa klabu ya Motherwell ya Uskochi James Scott, 19. (Team Talk)

Tetesi za Jumatatu

Real Madrid na Barcelona zinatarajiwa kushindana pakubwa kuwania kumvutia meneja Jurgen Klopp na mlinzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Liverpool. (AS, kupitia Star)

Manchester United imejitolea kumfanya kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, kuwa mcheza soka anayelipwa pakubwa katika ligi kuu ya England katika kumshawishi kusaini mkataba mpya wa muda mrefu (Times)

Christian Eriksen anapuuzia mkataba mpya anaopendekezewa na Tottenham wakati wakala wa mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 27akishughulikia uhamisho kwenda Real Madrid msimu ujao wa joto. (Marca, kupitia Express)

Mchezaji wa kiungo cha mbele Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, na kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid, baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chelsea mwenye miaka 28, kuhusishwa na uhamisho kwenda Uhispania. (Sun)

Eden Hazard, na kipa Thibaut Courtois, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid

Huenda Real Madrid ikamkabidhi mchezaji wa kiungo cha kati Toni Kroos, kwa Manchester United ili kwa upande wake ijipatie mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26 Paul Pogba. (FourFourTwo)

Arsenal inakaribia kufanikiwa kumsajili kijana wa Sunderland Logan Pye baada ya mchezaji huyo wa miaka 15 kuhusishwa ma uhamisho kwenda katika ligi kuu ya England wakati wa msimu wa joto. (Sun)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United, Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, yuko kwenye rada ya Juventus huku kukiwadia kinachowezekana kuwa ni mageuzi ya Januari. (Mirror)

Baada ya kuwasajili wachezaji 12 katika uhamisho wa msimu wa joto, mipango imeidhinishwa kwa Aston Villa kushughulika kwa mara nyingine katika dirisha la Januari. (Birmingham Mail)

Manchester United ilituma mawakala kumchunguza mshambuliaji wa Kosovo, Vedat Muriqi, mwenye umri wa miaka 25, wakati alipofunga dhidi ya timu ya England huko Wembley Jumanne usiku. (Express)

Meneja wa Arsenal, Unai Emery amefichua kwamba alikuwa na Javi Gracia wakati Watford ilipomfuta kazi. (Metro)

Bingwa wa Manchester United Gary Neville amesema anaweza 'kukimbia maili moja' iwapo atapewa kazi ya U meneja Old Trafford. (Manchester Evening News)

Chirwa na Djodi wanacheza kwa kuelewana kutokana na Djodi kuwa na uwezo wa umiliki mpira kwa hali ya juu ambapo akisaidiana na Chirwa mwenye nguvu basi mabeki wa timu pinzani huwa wanapata tabu.

Dar es Salaam. Washambuliaji Donald Ngoma na Shaban Idd Chilunda wameanzia benchi wakati Azam FC ikishuka uwanjani kusaka ushindi dhidi ya Triangle United katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika mchezo huo kocha Ettiene Ndayiragije ameamua kuwaweka benchi Ngoma na Chilunda akiwaanzisha nyota wake Richard Djodi na Obrey Chirwa.

Tangu Ndayiragije atue Azam msimu huu Ngoma ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Kombe la FA.

Chirwa na Djodi wameonyesha maelewana mazuri tangu mchezo uliopita dhidi ya Fasil Kenema ambao Azam ilishinda nyumbani.

Katika eneo la kiungo Frank Domayo leo ataanza pamoja na Salum Abubakar wakiwa na jukumu la kuilinda ngome yao huku wakipitisha pasi za mwisho kwa washambuliaji wao.

Kikosi cha Azam: Razack Abarola, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Yakub Mohamed, Frank Domayo, Salum Abubakari, Idd Seleman ‘Nado’, Richard Djodi, Obrey Chirwa na Emmanuel Mvuyekure.

Wachezaji wa akiba Mwadini Ally, Mudathir Yahya, Idd Kipagwile, Donald Ngoma, Masoud Abdallah, Shaban Chilunda na Oscar Masai.


Bocco Arejea na Ujumbe wa Kufurahisha Simba

JOHN Bocco ambaye ni nahodha wa Simba ametamba watachukua ubingwa wa ligi kuu na ule wa michuano wanayoshiriki ili kujipoza machungu ya kutolewa mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bocco ambaye hajacheza mechi mbili za ligi kuu ambazo Simba wameshacheza mpaka sasa kutokana na kuwa majeruhi, amesema watapambana wachukue makombe hayo baada ya kutupwa nje na UD do Songo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali kabisa.

Bocco ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa sasa wanaweka mikakati ya kutwaa makombe hayo hasa la ligi ili wapate nafasi tena ya kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa ambapo msimu uliopita walifika hatua ya robo fainali.

“Kweli tulikuwa na hali ya huzuni kwa wachezaji hasa baada ya kuondolewa mapema jambo ambalo hatukuwa tumelitarajia kabisa.

“Lakini kwa sasa tumepanga kuchukua mataji yote ili kupata nafasi ya kurejea tena kimataifa lakini pia kuwafurahisha mashabiki wetu baada ya kutokea kwa hali hiyo,” alisema Bocco ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azam aliyejijenga na kuacha kivuli chake kwenye klabu hiyo.

MAN United inauwezekano wa kukosa wachezaji sana katika mchezo wao wa leo dhidi ya Leicester City hiyo ni baada ya kuelezwa kuwa Paul Pogba na Anthony Martial wataukosa mchezo huo.

Kipute hicho cha Premier League kitapigwa kwenye Uwanja wa Old Traff ord ambapo Pogba ana majeraha ya kifundo cha mguu na ndiyo maana alikosa hata michezo ya timu yake ya taifa ya Ufaransa wiki iliyopita.

Wachezaji wengine wa United ambao wapo hatarini kuukosa mchezo huo ni Luke Shaw (nyama za paja), Diogo Dalot (nyonga), Jesse Lingard (mgonjwa) na Aaron Wan-Bissaka (mgongo) huku Eric Bailly akiwa nje muda mrefu kwa jeraha la goti.

Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer yupo katika presha kubwa kwa kuwa timu yake imepata ushindi mmoja tu katika mechi nne za ligi hiyo msimu huu.

MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
Pongezi kwa mshambuliaji aliyerejeshwa kikosini baada ya kuachwa kwa miaka kadhaa aende kupandisha kiwango chake kufuatia kuibuliwa timu ya vijana ya klabu, ‘Simba B’ Miraj Athumani ‘Madenge’ ama ‘Shevchenko’, au Sheva aliyefunga bao la ushindi akitokea benchi. 
Na hiyo ni baada ya Simba SC kutangulia kwa bao la mshambuliaji kinara wa mabao, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere aliyefunga bao la kwanza dakika ya 19 akimalizia krosi ya kiungo mpya, Msudan Sharaf Elidn Shiboub.  

Miraj Athumani ‘Madenge’ (katikati) baada ya kuifungia Simba SC bao la ushindi kufuatia kutokea benchi  

Mtibwa Sugar wakasawazisha bao hilo dakika ya 21 kupitia kwa mshambuliaji wao chipukizi, Riphat Msuya aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo Ismail Mhesa. 
Na dakika saba tu baada ya kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga uwanajani, Miraj akaifungia Simba SC bao la ushindi dakika ya 69 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Shiboub. 
Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Zubery Katwila ikapata pigo dakika ya 81 baada ya beki wake, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Henry Joseph Shindika dakika nne baadaye. 
Ushindi huo unaofuatia ushindi mwingine wa 3-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa kwanza, unaifanya SImba SC inayofundishwa na Mbelgiji Patrick Aussems ifikishe pointi sita na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, wakati Mtibwa wanapoteza mechi ya pili na zote ugenini, kufuatia kuchapwa 3-1 na Lipuli FC kwenye mchezo wa kwanza mjini Iringa. 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Tairone Santos, Gerson Fraga, Clatous Chamadk/Francis Kahata dk79, Muzamil Yassin, Meddie Kagere, Sharaf Shiboub/Jonas Mkude dk90 na Hassan Dilunga/Miraj Athumani ‘Madenge’ dk62.  
Mtibwa Sugar; Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/Henry Joseph dk85, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’, Ally Makarani, Riphat Msuya, Ismail Mhesa/Abdul Haule dk81, Awadh Juma na Haruna Chanongo/Omar Hassan dk68. 
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Coastal Union waliutumia vyema uwanja wa nyumbani, Mkwakwani mjini Tanga kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC, mshambuliaji chipukizi Ayoub Lyanga akianza kumsetia Shaaban Idd kufunga la kwanza dakika ya 61 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 72 akimalizia pasi ya Hassan Kibailo.

Barcelona imekuwa ikiteseka sana kwa kucheza bila ya huduma ya Messi, ambapo wameshinda mara moja tu katika mechi nane alizokosa, ukijumlisha na zile za Novemba mwaka jana.

Barcelona, Hispania. Lionel Messi amewekwa kando kwenye kikosi cha Barcelona kitakachochuana na Valencia wikiendi hii, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kama Muargentina huyo atakuwa fiti kukipiga kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kuwa majeruhi.

Messi, 32, bado hajaichezea mechi yoyote Barcelona msimu huu na ataendelea kuwa benchi kutokana na maumivu ya misuli ya kigimbi aliyopata kwenye kipindi cha mapumziko ya majira ya kiangazi.

Barcelona imekuwa ikiteseka sana kwa kucheza bila ya huduma ya Messi, ambapo wameshinda mara moja tu katika mechi nane alizokosa, ukijumlisha na zile za Novemba mwaka jana.

Kwa msimu huu, Barca wamekusanya pointi nne tu katika mechi zao tatu walizocheza kwenye La Liga bila ya huduma ya staa huyo. Kocha wa miamba hiyo ya Nou Camp, Ernesto Valverde alisema kwamba mshindi huyo mara tano wa Balon d'Or alipaswa kuwa fiti baada ya mapumziko ya mechi za kirafiki.

Lakini, kwa mazoezi ya Jumanne na Jumatano, Messi alionenkana akifanya kivyake kwa sababu bado hajapona vizuri. Kutokana na hilo, Messi hatarajiwi kuonenkana uwanjani kesho Jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Valencia. Taarifa zaidi zinadai kwamba kocha Valverde hataki pia kumhatarisha Messi afya yake kwa kumpanga kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund.

Taarifa za karibuni zimedai kwamba kwenye mkataba wa Messi kuna kipengele kinachomruhusu kuondoka bure mwishoni mwa msimu. Mkataba wa sasa wa staa huyo utakomea 2021, huku Barca wakidaiwa kuwa na mpango wa kumpa Messi mkataba wa maisha.

KIUNGO staa wa Simba, Claytous Chama jana alitumia muda mwingi mazoezini kudili na tatizo la Aishi Manula kufungwa mabao kwa mashuti ya mbali.

Chama alichukua mpira na kukaa nao katikati ya uwanja kumfanyia mazoezi kipa huyo kwa dakika kadhaa na baadaye akamuonyeshea dole akimaanisha kwamba ameanza kuimarika.

Manula msimu uliopita ambapo Simba iliruhusu mabao ya kufungwa 15 kati ya hayo Manula aliyofungwa yalikuwa ni yale ya nje ya 18 kama ambavyo alifungwa na mshambuliaji wa Alliance Zabona Khamis kwenye ushindi wa mabao 5-1 pia hata msimu huu mbele ya JKT Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 3-1 alitunguliwa bao la mbali.

Kwenye mazoezi yaliyofanyika jana viwanja vya Gymkhana baada ya Kocha wa Makipa Mwarami Mohamed kumaliza programu yake alimshtua Chama na kumpa mpira amalize kazi.

Chama bila hiyana akiwa katikati ya uwanja alianza kumpigia mashuti makali Manula ambaye alipangua mashuti mawili kati ya manne huku mawili akiyapaisha.

Habari kutoka kwenye benchi la ufundi ni kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu mpaka Manula atakapoimarika.

ILIPOISHIA juzi Jumanne katika makala haya yanayomhusu mwanachama na mmoja wa viongozi wa Yanga, aliyeibukia kutoka kuwa dereva hadi meneja.

Juzi tuliwaletea mambo mbalimbali yanayofanya atembee kifua mbele kulitumikia chama hilo, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza alivyoishia kulazwa baada ya kichapo walichokipata kutoka Simba na alivyojiweka rehani ili timu iachiwe ikakipige katika michuano mbalimbali..SASA ENDELEA

YANGA ILIMFILISI

Wakati kuna mashabiki wanatoa maneno makali kwamba wanaumizwa na matokeo mabaya ya Yanga na kuwatukana wachezaji, makocha na viongozi kitu ambacho hakina msaada kwa timu, kwa Hafidh Saleh ni tofauti kwani yeye yupo tayari kutumikia kiasi chake cha pesa kwa ajili ya timu ili tu iweze kuwa na mazingira mazuri.

Hafidhi anasema hakumbuki ulikuwa ni mwaka gani lakini timu ilikuwa chini ya Kocha Raoul Shungu ambaye alipambana kuhakikisha anakaa sehemu nzuri yeye pamoja na baadhi ya wachezaji kwa kuwapangia nyumba nzima ya kuishi.

“Shungu na wachezaji Method Mogella, Willy Martin, Sekilojo Chambua, Zakaria Kinanda na nyota wengine sikumbuki majina yao niliwapangia nyumba nzima yenye thamani ya laki tisa ambayo miaka hiyo ningeweza kununua hata viwanja vitatu lakini sikufanya hivyo na kuamua kuwapangia wachezaji kutokana na mapenzi niliyokuwa nayo kwa Yanga,” anasema.

“Kuhusu kufilisika kwa ajili ya klabu hiyo, siwezi kusema hivyo kwani nilikuwa nafanya kwa mapenzi na nilikuwa nafurahia kuona timu inakuwa katika mazingira mazuri, nilikuwa sipendi timu ipitie katika shida nilichokuwa nakipata katika biashara yangu nilikuwa tayari kukiwekeza Yanga,” anasema.

“Wengi wanasema kuhusiana na maisha yangu kuyumba kuwa Yanga imechangia, inaweza ikawa sababu lakini sidhani kama hilo lina ukweli, kwani wapo wengi wanaotumia fedha zao kwa ajili ya Yanga. Hii timu imenisomeshea wanangu, hivyo sioni shida nikiwanacho nishindwe kutoa kwaajili ya timu,” anasema.

“Nimefanya kazi chini ya viongozi wanne hadi sasa nilianza na Emmanuel Madega, Llyod Nchunga, Yusuf Manji na sasa Dk. Mshindo Msolla viongozi wote hao nimefanya nao kazi vizuri na kila mmoja alikuwa na mafanikio aliyoiachia klabu,” anasema na kuongeza:

“Manji sitamsahau katika uongozi wake, kwani aliifanyia mambo makubwa klabu alikuwa na mkono wa utoaji, alipambana na ndiye aliyeiingiza timu yetu mara mbili katika makundi tukiwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho,” anasema.

“Yanga kufikia mafanikio hayo ilitokana na usajili aliokuwa anaufanya alikuwa anasajili wachezaji wenye uwezo ambao waliweza kuipa timu mafanikio kwa kutwaa ligi mara tatu mfululizo na kushiriki mashindano ya kimataifa na kufika hatua ya makundi mara mbili,” anasema Hafidh.

“Madega pia aliipa ubingwa Yanga wa ligi na wa Afrika Mashariki hivyo pia namkumbuka kwa uongozi wake bora chini yake nisiwe mchoyo wa fadhila wote ni watendaji wazuri na ndio maana Yanga ipo hadi sasa nikimuelezea mmoja mmoja kwa uzuri sitamaliza leo,” anasema.

“Yanga imefanikiwa kuwasajili nyota wa kimataifa kutoka katika mataifa mbalimbali wengi walifanya mambo makubwa na nimefanya nao kazi vizuri nikiwa kama meneja, nitaendelea kuwakumbuka kwa mazuri na hata mabaya kwani hakuna mwanadamu asiyekosea,” anasema na kuongeza kuwa:

“Miongoni mwa mastaa waliopita Yanga nikiwa meneja miaka ya nyuma ni pamoja na Emmanuel Okwi, Donald Ngoma, Haruna Niyonzima, Yaw Beko, Davies Mwape, Hamis Kiiza na wengine wengi nikianza kutaja hapa sitamaliza Yanga imepitiwa na nyota wengi sana na walikuwa bora,” anasema.

“Soka la Tanzania linakuwa na limekuwa ni ajila kwa vijana wengi wanaojitambua sasa ni muda wa Serikali kuwekeza katika michezo kwa kuandaa bajeti ambayo itadili na michezo tu, ikiwa ni sambamba na kuendeleza michezo mashuleni ambako ndio kuna vipaji vingi vinashindwa kuendelezwa kutokana na kukosa maendeleo ya kusimamiwa.

“Michezo mashuleni imerudi lakini haisimamiwi vizuri ili kuwa bora na kuweza kutoa nyota wengi ambao wanaweza kuwa na chachu kwa timu yetu ya taifa ni kuweka bajeti ambayo inaweza kuwapa morali wachezaji na hata waalimu wanaowafundisha.

“Nikipata nafasi ya kuonana na Waziri wa Utamaduni, Michezo, Sanaa, Dk. Mwakyembe naweza kumwambia arudishe morali mashuleni kuwe na mashindano mbalimbali kama ilivyokuwa miaka ya nyuma lengo ni kuona vipaji vilivyopo mashuleni vinaendelezwa,” anasema.

“Naishi soka napenda sana mpira hata nikiwa nyumbani muda wangu wa mapumziko huwa nafuatilia mpira, mimi ni shabiki mkubwa wa Man United ambayo imekuwa ikizungumzwa sana sikuizi kutokana na matokeo yake, hiyo ndio timu yangu wakati wote,” anasema na kuongeza : “Timu yangu ya Ligi Kuu ya England ni nzuri ningekuwa na uwezo ningembadilisha kocha, ningependa Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino ndiye angeinoa Man United kutokana na mfumo wake wa ufundishaji kuendana na namna timu yetu inavyocheza kama sio yeye hata Kocha Pep Guardiola anafaa.

“Kukiwa hakuna mechi siku hiyo nitakaa kusikiliza muziki mimi ni Team Kiba mbali na muziki huo napenda ule wa kizamani, nawapenda Msondo Ngoma huwa nasikiliza nyimbo zao, mara baada ya kumaliza burudani, basi nitaanza kufuatilia maendeleo ya wanangu kimasomo,” anasema.

“Kuhusiana na shughuli za nyumbani naomba niwe muwazi sina ninachoweza kukifanya zaidi ya kuchemsha chai na mayai.

“Sijui kupita hiyo kazi huwa namuachia mke wangu, sijawahi kumsaidia kwa lolote ni kutokana na kutofahamu, sina maana mbaya kwamba sio jukumu langu.

“Mke wangu ana busara ananielewa kulingana na mapungufu hayo sio bepari kwamba naamini kupika, kuosha vyombo au kufanya usafi ni kazi ya mwanamke, la hasha sasa usawa ni kwa wote lakini kwangu ni tofauti kutokana na kutoweza majukumu hayo.

“Nimelelewa katika familia yenye watoto wengi wa kike ambao walikuwa wanafanya majukumu hayo kwa usawa wakimsaidia mama, nadhani hiyo inaweza ikawa sababu ya mimi kushindwa kujifunza mambo hayo ya kupikapika na nashindwa kumsaidia mke wangu,” anafunguka Hafidhi ambaye ni mtu mtaratibu sana.

Zesco imejengwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa, ambao Yanga wanapaswa kuwa makini nao kwa dakika zote tisini ili kuanza vyema safari yao ya kwenda hatua ya makundi

Dar es Salaam. JUMAMOSI hii Yanga itashuka katika Uwanja wa Taifa katika mchezo wake wa hatua ya pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia, kutafuta tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi hiyo.

Yanga ilifika hatua ya pili baada ya kulipiza kisasi kwa kuwaondosha Township Rollers kwa mabao 2-1 katika michezo yote miwili ya Ligi hiyo. Township iliwahi kuiondosha Yanga misimu miwili iliyopita.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa wa aina yake na wakipekee hasa kutokana na timu hiyo kuwa ndiyo pekee kutoka nchini inayoshiriki michuano hiyo baada ya watani wao Simba kutolewa na UD Songo wiki mbili zilizopita.

Yanga imekuwa ikitumia vyema michezo ya maandalizi katika ziara yao waliyofanya hivi karibuni kanda ya ziwa kwa lengo la kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa.

Katika ziara hiyo Yanga imecheza michezo miwili, dhidi ya Pamba Fc mchezo uliosiha kwa sare ya 1-1 na dhidi ya Toto African ulioisha kwa Yanga kushinda mabao 3-0, huku mshambuliaji wao mpya David Molinga akibuka kidedea kwa kufunga mabao mawili katika mchezo huo.

Pamoja na hilo, wapinzani wao Zesco sio wabaya kwani hata katika michezo mitatu waliyocheza msimu huu wameshinda yote licha ya kwamba ni kwa ushindi mwembamba.

Katika mchezo wao wa kwanza wa ligi walishinda bao 1-0 dhidi ya Zanaco na kushinda tena mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Green Mamba Fc kwa mabao 3-0 katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.

Zesco imejengwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa, ambao Yanga wanapaswa kuwa makini nao kwa dakika zote tisini ili kuanza vyema safari yao ya kwenda hatua ya makundi. Hawa ndiyo wachezaji watano tishio ambao Yanga wanapaswa kuhakikisha wanawachunga kwa dakika zote.

JESSE WERE

Huyu ni mshambuliaji raia wa Kenya katika misimu yake miwili akiwa na Tusker ya nchini kwao alifunga mabao 34, katika michezo yote baada ya kujiunga na Zesco 2016, ameendelea kuwasha moto. Chini ya kocha George Lwandamina, Were amekuwa chaguo la kwanza na mwenye kuaminika.

Sifa za mchezaji huyo aliyewahi kutakiwa na Kaizer Chief, ana kasi ya ajabu na mwepesi wa kufanya maamuzi ndani ya eneo la hatari, Yanga inapaswa kuwa makini na mchezaji huyo aliyefunga bao pekee katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Green Mamba Fc.

UMARU KASUMBA

Ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika kikosi hicho, Kasumba ameanza vizuri kwa kufunga bao moja katika mchezo wa marudiano kufuzu Ligi ya Mabingwa dhidi ya Green Mamba Fc. Kasumba mwenye umri wa miaka 25 ni mrefu mwenye sentimita 181 ni mzuri kwa mipira ya vichwa hivyo Yanga wanapaswa kuhakikisha hawaruhusu ukigwaji wa krosi.

Msimu wa 2018/2019 alishika nafasi ya tatu kwa ufungaji bora baada ya kufunga mabao 17, baada ya msimu kumalizika alipata ofa ya kwenda kufanya majaribio nchini Ujerumani na kushindika na kuangukia Zesco United baada ya Nkana Fc kumkosa ambao pia walikuwa wakimuhitaji.

JOHN CHING’ADU

Kiungo huyu mshambuliaji raia wa Zambia ni mzuri kwenye kupiga mashuti yenye macho, pamoja na kugawa pasi za mwisho awapo uwanjani, ni mchezaji ambaye kila kona ya uwanja unamuona katika kuhakikisha anasaidia timu yake.

Yanga wanapaswa kuhakikisha mchezaji huyo hapigi shuti lolote na wala kutoa pasi ya mwisho inayoweza kuleta madhara kwa upande wao. Kiungo huyo alifunga bao moja katika mchezo wa kufuzu Ligi ya Mabingwa dhidi ya Green Mamba Fc.

MARCEL KALONDA

Beki huyo wa kati raia wa Congo, sifa kubwa aliyonayo ni upigaji wa vichwa, hii inatokana na urefu alionao unakadiriwa kufika sentimita 188, njia pekee ya kumzuia, Yanga wanapaswa kuhakikisha hawaruhusu kona au mpira ya adhabu na kumkaba muda wote na kuhakikisha haruki.

Kalonda ni mchezaji pekee mdogo 21, kwenye kikosi hicho na kocha Lwandamina ameonyesha kuwa na imani naye katika michezo miwili iliyopita na mmoja wa ligi uliopigwa wiki tatu zilizopita dhidi ya Zanaco.

ENOCK SABUMUKAMA

Alifunga bao pekee kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Zanaco, sifa kubwa ya mchezaji huyo ni kumiliki mpira na kutoa pasi za uhakika kwa wakati sahihi.

Yanga inapaswa kuhakikisha hawamruhusu kiungo huyo kumiliki mpira kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanampa faida ya kupenyeza pasi kwa uhakika hali itakayoweza kuwagharimu.


Sura Mpya Kibao Kuivaa Mtibwa Taifa Kesho

KESHO Simba itatupa kete yake ya pili kucheza na Mtibwa Sugar lakini safari hii sura nyingi mpya zitaonekana kwenye kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu wa mazoezi ya jana, inaonekana kwamba Aussems atapangua kikosi kitakachoivaa Mtibwa ili kuimarisha ufanisi wa Simba na kuonyesha dhana ya kikosi kipana. Jana alichezesha vikosi viwili mazoezini.

Kikosi cha kwanza kilikuwa kinaundwa na Aishi Manula ambaye ni mlinda mlango na upande wa mabeki ilikuwa ni Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Shomari Kapombe, Fraga Vieira, kwa upande wa viungo ni Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Fraga Vieira, Clatous Chama, Shiboub na mshambuliaji alikuwa ni Miraji Athuman.

Kwa upande wa kikosi cha pili kiliundwa na Beno Kakolanya ambaye alikuwa ni mlinda mlango kwa upande wa mabeki Pascal Wawa, Haruna Shamte, Kennedy Juma na Gadiel Michael upande wa viungo wakiwa ni Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Francis Kahata na kwa upande wa washambuliaji akiwa Deo Kanda na Rashid Juma.

Mwishoni kabisa alimfanyia mabadiliko Jonas Mkude na Fraga Vieira, Tshabalala alichukua nafasi ya Gadiel.

Aliyekuwa kocha wa timu ya kandanda nchini Tanzania Emmanuel Amunike amelishtaki shirikisho la soka la Tanzania TFF kwa shirikisho la mchezo huo duniani FiFa akilalamikia kutolipwa haki yake.

Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania lililonukuu mtandao wa Complete Sport.com na Punching.com , Kocha huyo raia wa Nigeria ameamua kuwasilisha malalamishi hayo kwa Fifa ili kutafuta haki yake.

Amunike alitimuliwa na shirikisho la soka la Tanzania baada ya tanzania kupata matokeo duni katika kombe la mataifa ya Afrika .

''Nimewasiliana na Fifa juu ya hilo jambo . Sio Swala la kupiga kelele , lakini nina imani watalitazama na kuamua iwapo ni sahihi mtu kutolipwa baada ya kufanya kazi'', Amunike alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema.

Kocha huyo ambaye mkataba wake ulivunjwa mwezi Julai mwaka huu amerejea Uhispania ambako makazi yake ya kudumu yapo.

Kwa mujibu wa Mwananchi , TFF waliafikia uamuzi huo wa kuvunja mkataba na kocha mchezaji huyo wa zamani wa Nigeria baada ya taifa Stars kuandikisha matokeo mabaya katika fainali ya Afcon 2019 zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19.

Katika fainali hizo taifa Stars ilishika mkia kwenye kundi C lililokuwa na Senegal, Kenya, na Algeria baada ya kupoteza mechi zote ta

Kushindwa kwao na majirani zao kenya ndio kulikohuzunisha wengi kwa kuwa walipoteza uongozi waliokuwa nao wa 2-0 kufikia kipindi cha mapumziko.

Na kufuatia matokeo hayo Amunike alisea kwamba timu hiyo ilihitaji uzoefu wa mashindano makubwa na kwamba wachezaji walihitaji kushiriki katika ligi zenye ushindani mkubwa ili kuweza kuimarika.

Kocha huyo ambaye mwenye umri wa miaka 47 ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka klabu ya Sudan ya A; Khartoum mnamo mwezi Machi aliandikisha mkataba wa miaka miwili na taifa hilo la Afrika mashariki akichukua nafasi yake Saulm Mayanga.

Amunike alishinda kombe la Afrika akiichezea Super Eagles ya Nigeria 1994 na mshindi wa dhahabu ya Olimpiki miaka miwili baadaye.

Katika kipindi chake cha mchezo aliichezea, SC Zamalek, Sporting \lisbon, na Barcelona ijapokuwa majeraha yalimzuia kuafikia ndoto yake mjini Catalonia.

Winga huyo wa zamani alianza ukufunzi na timu ya nigeria isiozidi wachezaji wa miaka 17 2014 na kushinda kombe la dunia la kinda hao mwaka mmoja baadaye.

Tiketi zinapatikana kwa bei ya Sh 3,000, 5,000 na 10,000 katika vituo vya Dar Live, Chamazi Complex, kwenye duka la Ice Cream, na pale Azam Shop.

Dar es Salaam. Mashabiki wa AzamFC wataishuhudia mechi mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle United FC ya Zimbabwe kwa kiingilio cha Sh3,000 na Sh 10,000 kwa VIP kwenye Uwanja wa Chamazi Complex.

Tiketi zitaanza za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo vya Dar Live, Chamazi Complex, kwenye duka la Ice Cream, na pale Azam Shop.

Afisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd alisema mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili hasa katika kusaka nafasi ya kujiweka vyema wanapopata matokeo mazuri katika mchezo huo.

"Hii ni nafasi nyingine kwa Watanzania kuisapoti timu yao ili izidi kupeperusha bendera ya taifa katika mashindano hayo," alisema Idd.

Azam inayonolewa na Kocha Etienne Ndayiragije imekuwa na matokeo mazuri zaidi inapocheza uwanja wake wa nyumbani kuliko ugenini hivyo rekodi hiyo inaonekana kuwabeba kuelekea katika mchezo huo wa Jumapili.

Ndayiragije na vijana wake walifanikiwa kutinga hatua hiyo kwa kuitoa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa uwiano wa mabao 3-2 baada ya ushidi wa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi Complex huku katika mchezo wa kwanza wakikubali kulala kwa bao 1-0, wakati wapinzani wao wakiitoa Rukinzo FC ya Burundi kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya suluhu katika mchezo wa mwisho.

Lionel Messi amepigiwa kura na kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa Kimataifa kwa mwaka 2019, kwenye tuzo za ESPY.

Tuzo za ESPY (Excellence in Sports Performance Yearly Award) zinazolenga kutambua Utendaji bora wa wanamichezo kwa kila mwaka. Ni tuzo zinatolewa kwa sasa na kituo cha matangazo ya runinga Amerika (ABC) na hapo awali ESPN.

Ikubukwe Messi alikuwa mfungaji Bora: Laliga (Mabao 36), Uefa Champions League (Mabao 10) na mfungaji bora Ulaya (mabao 51).

Ndani ya misimu yake miwili akiwa na El Jadida, Msuva ambaye alijiunga na timu hiyo Julai 2017, ameifungia jumla ya mabao 24, yakiwemo 13 ya msimu uliopita.

Dar es Salaam. Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Saimon Msuva amejiwekea malengo ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Morocco ambayo ni maarufu kama Batola Pro akiwa na klabu yake ya Difaa El Jadida msimu huu.

Msuva ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kilichoing’oa Burundi na kuingia hatua ya makundi ya kuwania nafasi ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, alisema ana uzoefu wa kutosha na Ligi hiyo hivyo ana kila sababu ya kutimiza ndoto yake.

“Huu utakuwa msimu wangu wa tatu kucheza Ligi ya Morocco, takribani kwenye kila msimu nilikuwa kwenye nafasi ya kuwa mfungaji bora, lakini kufanya vibaya kwa timu mwishoni mwa msimu kumekuwa kukiniangusha.

“Kama timu inapoteana ni ngumu kuendelea kufunga. Awamu hii naona kuna utofauti kuanzia kwenye maandalizi hadi kwenye aina ya wachezaji ambao wameongezwa, naamini itawezekana,” alisema mshambuliaji huyo wa pembeni.

Ndani ya misimu yake miwili akiwa na El Jadida, Msuva ambaye alijiunga na timu hiyo Julai 2017, ameifungia jumla ya mabao 24, yakiwemo 13 ya msimu uliopita.

Katika misimu yake miwili akiwa nchini Morocco, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, ameibuka kuwa mfungaji bora kwenye kila msimu kwa klabu yake ya Difaa huku pia akiwa mchezaji wa kigeni mwenye mabao mengi zaidi ndani ya misimu hiyo.

Akiwa na Yanga kabla ya kwenda Morocco, Msuva aliwahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya misimu miwili ambayo ni 2014/15 kwa kufunga mabao 17 na 2015/16 kwa mabao 14 akilingana na Abdulraham Mussa wa Ruvu Shooting.

Yanga inatarajia kuondoka Mwanza jioni kurudi Dar es Salaam kujiwinda na mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mwanza. Beki wa Yanga, Juma Abdul aliyekuwa amefiwa na mama yake leo ameungana na wenzake katika mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja Nyamagana, Mwanza.

Yanga ipo kambini Mwanza kujianda na mchezo wake wa kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ya Zambia utakaochezwa September 14, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Beki Abdul aliondoka kambini hapo kufuatia msiba wa mama yake mzazi uliotokea wiki moja iliyopita, leo ameungana na wenzake mazoezini  kujiandaa na mchezo huo.

Mbali na nahodha huyo msaidizi, wachezaji wengine walioungana na timu leo kwenye mazoezi ya mwisho kwenye kambi ya Mwanza ni kiungo Mohamed Issa na Kelvin Yondani waliokuwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichocheza dhidi ya Burundi.

Wachezaji wanne hawajafanya mazoezi ya leo ambao ni Kipa Farouk Shikhalo (Kenya)  na Patrick Sibomana (Rwanda) pamoja na Paul Godfrey na Issa Bigrimana ambao ni majeraha.

Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho jijini Mwanza kabla ya kupanda ndege leo jioni kurudi Dar es Salaam tayari kuwavaa Zesco katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika.

USHINDI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, umemkuna Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussem, huku akiwamwagia sifa wachezaji wa timu hiyo, wakiwamo kipa Juma Kaseja na beki wa kati, Kelvin Yondani, akitamani wangekuwa ni wa kikosi chake.

Stars iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kuwania kufuzu makundi ya kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazopigwa Qatar.

Katika mchezo huo wa juzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hadi dakika 120 zinamalizika, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza wa Septemba 4, nchini Burundi, hivyo mshindi kuhitajika kupatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penalti na Taifa Stars kushinda kwa matuta 3-0.

Shujaa wa mchezo huo, alikuwa ni Kaseja aliyeokoa penalti ya kwanza na nyingine mbili kwenda nje, huku Yondani akishirikiana na Erasto Nyoni kuwadhibiti washambuliaji wa Burundi waliokuwa wakiongozwa na straika anayekipiga Ulaya, Saido Berahino.

Akizungumza na BINGWA jana, Aussems alisema kuwa Kaseja na Yondani ni miongoni mwa wachezaji waliomkuna vilivyo, wengine wakiwa ni kocha wa Stars, Etienne Ndayiragije kwa kuwapa nafasi wachezaji wengine kadhaa kuonyesha uwezo wao.

Aussems alisema kikosi kilichocheza na Burundi ni tofauti na kile cha michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, iliyofanyika Juni hadi Julai, mwaka huu nchini Misri ambapo timu hiyo ilikuwa chini ya kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike.

“Nimeangalia mechi mwanzo mwisho, naipongeza sana Taifa Stars, imefanya kazi nzuri, wachezaji wamejituma kwa kucheza katika kiwango cha juu, ukiangalia kuna utofauti wa kikosi hiki na kile kilichokwenda AFCON kutokana na uwepo wa nyota wapya,” alisema.

Alisema mbali ya Kaseja na Yondani, wachezaji wake wanaotoka Simba, wamemfurahisha zaidi, hasa Nyoni na Gadiel Michael kwa jinsi walivyoonyesha ujasiri wa kupiga penalti.

“Nimefurahishwa na wachezaji wangu wa Simba, wamefanya kazi nzuri, nimeona penalti za Gadiel na Nyoni, wamepiga kwa umakini mkubwa na kuisaidia timu kusonga mbele,” alisema.

Alipoulizwa iwapo angetamani Kaseja au Yondani kuwapo katika kikosi chake, alisema kuwa hakuna kocha anayeweza kukataa kuwa na mchezaji mzuri kikosini kwake.

“Ni wachezaji wazuri na walifanya vizuri, hakuna kocha anayeweza kumkataa mchezaji mzuri, lakini binafsi najivunia na wachezaji waliopo katika kikosi changu cha Simba, ni wazuri na wana uwezo wa kuwapa mashabiki matokeo mazuri,” alisema.

Nyota wengine wa Simba walikuwapo katika kikosi cha Stars kilichoivaa Burundi ni Jonas Mkude, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Beno Kakolanya ambaye alikuwa benchi.

LIVERPOOL ENGLAND. SUPASTAA Sadio Mane alionekana kuwa mwenye hasira baada ya mshambuliaji mwenzake Mohamed Salah kushindwa kumpa pasi wakati yeye akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England ambapo Liverpool iliichapa Burnley 3-0 wikiendi iliyopita.

Staa huyo wa Senegal alitolewa muda mfupi tu baada ya tukio hilo, lakini hakuweza kuficha hasira zake, alionekana akibwatuka mbele ya benchi la ufundi na wachezaji wenzake kadhaa walimtuliza, akiwamo Roberto Firmino, Joe Gomez na James Milner.

Kocha Jurgen Klopp aliamua kulipuuzia jambo hilo, lakini video ya Roberto Firmino ikimwonyesha akicheka kutokana na jambo hilo ghafla ilipata umaarufu sana kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki nao wakavamia na kukuza mambo, wakidai kutakuwa hakuna uhusiano mzuri baina ya wawili hao, huku baadhi wakimshutumu Mo Salah kuwa ni mbinafsi.

Lakini huko nyuma mwezi Mei, muda mfupi kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mane alisema kitu kuhusu uhusiano wake na Mo Salah, katika mahojiano maalumu yaliyofanywa na gwiji wa Liverpool, Robbie Fowler. Haya ndiyo majibizano yao yalivyokuwa.

Fowler: Ok, swali hili nikiwa mshambuliaji mwenzako. Matokeo ni 0-0 hadi dakika ya mwisho ya mechi ya fainali, imepatikana nafasi. Nani ungetaka awe kwenye nafasi hiyo ya kufunga, wewe au Mo Salah?

Mane: Hahahaha! Mimi nataka ushindi tu! Mo anafunga, mimi nafunga, nahitaji kombe. Nadhani, ninachohitaji ni taji tu, wakati mwingine mambo mengi yamekuwa yakinikwaza. Anaweza kufunga, Mo wewe funga tu. Hadi tutakapopata taji, Mo afunge tu!

Fowler: Nadhani hili linafanya ufahamike zaidi jinsi ulivyo. Mimi sidanganyi, ningetaka niwe mimi!

Mane: Nataka kusema ukweli. Nataka taji, kama Mo yupo kwenye nafasi ya kumpunga nampa mpira, tunataka taji, hivyo afunge tu!

Fowler: Unaonekana kama ni mchezaji unayetaka kujitolea kwa ajili ya timu. Hivi unafurahia kwamba umekuwa huzungumziwi sana, wakati Mo anapata sifa tu kila siku, wewe unaichukuliaje hiyo?

Mane: Nadhani tangu msimu uliopita, hadi wakati huu, Mo amekuwa kwenye kiwango bora sana. Kama unataka kushinda kitu kwenye timu, bila ya shaka unahitaji wachezaji wa aina hii. Hiyo unatumia nguvu iliyopo kwenye timu. Mo alikuwa mfungaji bora, alikuwa akifunga na kutusaidia. Kama asingekuwapo, pengine tusingefika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa sasa amekuwa akifunga mabao mengi muhimu.

Kwangu mimi muhimu ni kushinda kitu. Mo anaweza kufunga, au Bobby Firminho au mimi, haijalishi. Nadhani kama timu tumekuwa tukifanya kila kitu kitimu, tunasaidiana. Kipa, mabeki, viungo, kila mmoja.

Fowler: Watu wanasema huko kuna ushindani mkubwa baina yetu na hamna urafiki kabisa, kweli hakuna tatizo hapo?

Mane: Hakuna. Maneno kama hayo au vitu vingine vyovyote vimekuwa vikitokea sana kwenye soka. Mimi sijali, kama nimefunga au sijafunga ilimradi timu imeshinda. Baadhi ya watu wanataka kusema tuna upinzani, lakini nadhani hilo ndilo linalofanya mchezo wa soka uwepo, upinzani.

Lakini, hilo halina maana kwangu. Kwa kusema ukweli!

Farid ambaye alijiunga na CD Tenerife ya  Ligi Daraja la Kwanza Hispania maarufu kama Segunda, amefichua hilo wakati akiwa kambini kabla ya mchezo wa jana dhidi wa Burundi wa kuwania kufuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Qatar,  2022.

KIWANGO alichoonyesha winga wa Kitanzania, Farid Mussa kwenye mchezo wa makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Kenya kimeziweka njia moja klabu kadhaa barani Ulaya kusubiri huduma yake ifikapo Januari, mwakani.
Farid ambaye alijiunga na CD Tenerife ya  Ligi Daraja la Kwanza Hispania maarufu kama Segunda, amefichua hilo wakati akiwa kambini kabla ya mchezo wa jana dhidi wa Burundi wa kuwania kufuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Qatar,  2022.
Winga huyo alisema kuna zaidi ya timu tatu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili, hivyo Januari anaweza kuachana na chama lake la CD Tenerife na kujiunga na miongoni mwa timu hizo.
“Naweza kuondoka Januari CD Tenerife, ni zaidi ya asilimia 80 kwa sababu kuna timu ambazo zilivutiwa na uwezo wangu kipindi cha Afcon, nadhani ni muda sahihi kwangu kwenda kujaribu kwingine,” alisema mchezaji huyo katika mahojiano na Mwanaspoti.
“Nina shauku ya kucheza kwa mafanikio, nilichojifunza hapa naweza kukitumia huko ambako naweza kwenda. Zipo timu za Hispania na nyingine za mataifa mengine ya hukohuko Ulaya.”
Tangu ajiunge na CD Tenerife, Farid mwenye umri wa  miaka 23 amekuwa akitumika kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo ambacho kinashiriki Ligi Daraja la Tatu nchini humo ambayo inafahamika zaidi kama Tercera.
Mchezaji huyo alisema klabu hizo ambazo zinataka kumsajili zilivutiwa naye na uwezo ambao aliuonyesha kwenye mchezo wa Afcon, Juni 27 ambapo Taifa Stars ilipoteza kwa mabao 3-2 mbele ya Kenya.
Katika mchezo huo, Farid alionyesha kiwango cha juu kwa akishiriki kusababisha bao la kwanza ambapo  alipiga pasi akiwa katikati ya uwanja iliyomfikia Mbwana Samatta ambaye alipiga shuti lililochezwa na kipa wa Kenya kabla ya Saimon Msuva kumalizia kirahisi.
Kabla ya kutimkia Hispania, Farid alikuwa akikipiga Azam FC ya jijini Dar es Salaam na aliondoka nchini mwaka 2016.

Kwa mujibu wa taarifa  kutoka Ubelgiji huenda Mbappe akawa mrithi wa Mbwana Samatta ambaye anatazamiwa kuondoka KRC Genk kipindi cha usajili cha Januari, mwakani.

NYOTA wa timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’, Kelvin Pius John  ‘Mbappe’ yuko mbioni  kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anayoichezea nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.
Kwa mujibu wa taarifa  kutoka Ubelgiji huenda Mbappe akawa mrithi wa Mbwana Samatta ambaye anatazamiwa kuondoka KRC Genk kipindi cha usajili cha Januari, mwakani.
Kutokana na kanuni za kisheria za kuingia na kukaa Ulaya hasa kutokana na udogo wa umri wake,  itambidi kinda huyo wa Kitanzania aingie Ubelgiji kama mwanafunzi ambaye atakuwa akicheza soka kwenye kituo cha chama hilo.
Mbappe huyo wa Tanzania, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa nchini akiwa na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, aliwahi kufanya majaribio ya kujiunga na HB Køge ya Denmark.
Kinda huyo pia aliwahi kufanya majaribio na kufuzu nchini  Afrika Kusini kwenye klabu ya Ajax Cape Town huku akitazamwa na kipa wa zamani wa Manchester United,  Edwin van der Sar.
Edwin van der Sar  alienda Afrika Kusini kutokana na uhusiano uliopo baina ya Ajax ya nchini kwao Uholanzi ambayo alikuwa akiifanyia kazi na timu hiyo yenye maskani yake Cape Town.
Dili la kinda huyo wa Kitanzania, linatarajiwa kutangazwa rasmi ndani ya mwezi huu baada ya kulitumikia Taifa katika  Mashindano ya Cecafa U20 yatakayofanyika   nchini Uganda.
Mbappe ataungana na Faissal Boujemaoui wa
Morocco ambaye alikuwepo nchini hapa akilitumikia Taifa lake kipindi cha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri  chini ya miaka 17 zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

NAHODHA na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burundi, Saido Berahino, amemsifia beki wa Taifa Stars, Kelvin Yondani na kikosi hicho kwa ujumla, baada ya kutinga hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia, zitakazofanyika Qatar mwaka 2022.

Stars ilitinga hatua hiyo kwa kuichapa Burundi mikwaju ya penalti 3-0, ikiwa ni baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1, matokeo kama ya mechi ya kwanza iliyopigwa Septemba 4, mwaka huu, mjini Bujumbura.

Berahino alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Burundi waliokosa mkwaju wa penalti kati ya watatu waliopiga.

Akizungumza na BINGWA baada ya mchezo huo wa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Berahino alisema yeye na wenzake watakuwa wakiendelea kuipa sapoti Stars katika safari yake ya kusaka tiketi ya Kombe la Dunia.

“Taifa Stars ni sehemu ya nchi za Afrika Mashariki, tumefurahi kwa upande wetu, hatukuwa na bahati, tulipata nafasi na kushindwa kuzitumia, hii ni sehemu ya mchezo, mechi ilikuwa nzuri na kila mtu alifurahia,” alisema Berahino.

Berahino alipoulizwa juu ya mchezaji wa Stars aliyemvutia, alijibu: “Wachezaji wote wapo vizuri, ila kwa upande wangu Samatta namkubali zaidi, japo pia yupo yule jezi namba tano (Yondani), alitupa wakati mgumu sana, anajua kukaba, ni beki mzuri sana kwa kweli pamoja na yule mwenzake (Erasto Nyoni).”

Berahino aliyewahi kutamba na Stoke Cityu ya Ligi Kuu England, kwa sasa anakipiga katika klabu ya S.V. Zulte Waregem ya Ubelgiji, akiwa ligi moja na Samatta anayeichezea KRC Genk.

Bigirimana alisema kutokana na maumivu hayo ya paja ameshindwa kuyaelewa na kuna wakati anajiona yuko vizuri lakini baadaye mambo hubadilika na kuwa mabaya zaidi.

YANGA inaendelea na maandalizi yake kujiwinda na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ya Zambia lakini ukiacha Patrick Sibomana ambaye yupo na timu ya taifa yake kuna mshambuliaji mmoja amejiondoa mapema katika kikosi hicho.
Mshambuliaji Issa Bigirimana hayupo katika kikosi cha Yanga sasa akibaki jijini Dar es Salaam ameliambia Mwanaspoti hataweza kuingia kambini kufanya maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Zesco.
Bigirimana raia wa Burundi jana Jumapili alikuwepo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kama shabiki akiliangalia taifa lake la Burundi akisema maumivu ya paja ndiyo yanayomtesa kwa sasa.
Bigirimana alisema kutokana na maumivu hayo ya paja ameshindwa kuyaelewa na kuna wakati anajiona yuko vizuri lakini baadaye mambo hubadilika na kuwa mabaya zaidi.
“Sijaenda na timu nipo hapa Dar es Salaam kama unavyoniona naumwa nyama ndugu yangu,” alisema Bigirimana.
“Kwakweli nimekuwa sielewi haya maumivu yanatokea wapi, kwa sababu yananinyima raha. Kuna wakati najiona niko salama kabisa lakini baada ya muda yanarudi. Nikitaka kuanza mazoezi hali inarudi na kuwa mbaya zaidi,” alisema kwa masikitiko.
Aidha Bigirimana alisema kwasasa yuko katika mchakato wa kubadilishiwa daktari kwa ajili ya maumivu hayo ambayo tangu amefika hajacheza mechi yoyote ya kimashindano.
“Nimeambiwa kuna daktari mwingine nitapelekwa ili naye akaniangalie ndiyo nasubiri kuona mambo yatakuwaj.”
Akiwa kambini Morogoro katika maandalizi ya msimu mpya Bigirimana alikuwa moto akifunga mabao makali lakini hali ikabadilika alivyotua jijini Dar es Salaam.
Yanga  ya Kocha Mwinyi Zahera iko kwenye changamoto ya washambuliaji wake kutotumia nafasi katika mechi zake.
Inaamika kama straika huyo angekuwa fiti mambo yangebadilika na labda Yanga  isingekuwa na shida katika upachikaji wa mabao.
Mara nyingi makocha huwataka wachezaji wao hata wakiwa majeruhi kusafiri au kwenda kutazama mazoezi lakini kwa Bigirimana  imeshindikana kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi Maurizio Sarri kuzuia uhamisho wa nchezaji huyo wa Brazil. (Mail)

Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen msimu ujao iwapo Paul Pogba ataongeza kandarasi yake na Man United .

Eriksen mwenye umri wa miaka 27 atapatikana kwa uhamisho wa bila malipo kwa kuwa kandarasi yake inakamilika 2020. (Sky Sports)

Beki wa Real Madrid Sergio Ramos amemshauri Pogba, 26, kutoka Man United na kuhamia katika klabu hiyo ya Uhispania. (Express)

Chelsea imeanzisha mazungumzo na beki wa Itali Emerson, 25, kuhusu kandarasi mpya mpya. Winga wa England Callum Hudson Odoi 18 anakaribia kukamilisha mkataba mpya wa malipo ya £180, 000 kwa wiki katika mkataba wa miaka mitano.. (Express)

Tottenham iliwatuma wawakilishi ili kumtazama mshambuliaji wa Fenerbahce Vedat Muriqi, 25, akiichezea Kosovo wikendi iliopita.

Maskauti kutoka Lazio, Fiorentina na Napoli pia walikuwepo huku Muriqi akifunga katika ushindi wa Kosovo wa 2-1 dhidi ya Czech Republic. (Sabah, via Four Four Two)

Mlinda lango wa Manchester United David de Gea, 28, anakaribia kutia kandarasi mpya ambayo itampatia mshahara wa £290,000 kwa wiki ikiwa ni mshahaha anaolipwa Pogba. (Guardian)

Mchezaji wa timu ya Itali ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Paolo Nicolato amemwambia mshambuliaji wa Everton Moise Kean kujifunza kutokana na makosa baada ya kuwasili kuchelewa katika mkutano wa timu kabla ya mechi dhidi ya Ubelgiji.

Kean 19 aliwachwa nje kutoka katika kikosi cha Itali katika mechi za kimataifa za hivi karibuni (Gazzetta Dello Sport, via Sport Witness)

Tottenham ilitaka kumsaini kiungo wa kati wa Roma Nicolo Zaniolo, 20, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo kabla ya kumsaini Giovani lo Celso kwa mkopo badala yake. (Mail)

Wolves ilifeli kumsaini kiungo wa kati Leeds Kalvin Phillips msimu huu ,ilibainika baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kutia kandarasi mkataba mpya katika klabu hiyo.. (Football Insider)

Chelsea imeambia maajenti wake wakuu kwamba inaamini kwamba marufuku ya uhaimsho waliowekewa inayowazuia kununua wachezaji msimu huu itapunguzwa , ikimaanisha kwamba wanaweza kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 27, ametaja baadhi ya ukosoaji dhidi Steve Bruce na klabu hiyo kama upuzi na aibu. (Chronicle)

Klabu ya ligi ya Bundelsiga Paderborn huenda inataka kufanya jaribio la pili la kumsaini kiungo wa kati wa Crystal Palace Jairo Riedewald, 23, mnamo mwezi Januari baada ya kukosa uhamisho wa mkopo msimu huu . (Football.London)

Beki Jesus Vallejo, 22, aliyejiunga na Wolves kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la msimu huu anaweza kuuzwa na klabu ya Real Madrid msimu ujao. (Birmingham Mail)

Tamasha kwa jina A Cirque du Soleil kuhusu mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi liitaanza katika mji wa Catalan mwezi Oktoba. (Standard)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

Barcelona wanajiandaa kusaini mkataba na mshambuliaji wa mbele Lionel Messi, 32

Barcelona wanaandaa mkataba mpya wa mshambuliaji Lionel Messi, 32, ambao utambakisha nyota huyo Camp Nou kwa miaka iliyosalia ya maisha yake ya soka. (Mundo Deportivo via Mirror)

Chelsea inaweza kulazimika kumpa mkataba wa muda mrefu beki wake wa kushoto Mbrazil Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 25, ambaye kocha Maurizo Sarri anamyemelea kumpeleka Juventus. (Express)

Manchester United na Manchester City wapo mbioni kupambana kumsajili kiungo wa wa Benfica Florentino Luis mwenye umri wa miaka 20. (Star)

Paul Pogba

Kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27, aliamua kusalia Manchester United badala ya kuhamia Real Madrid kutokana na mkataba wa pauni pauni 150 wa udhamini wa michezo . (The Sun)

Beki wa timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk, 28, ameshangazwa na maneno kuwa atapewa ofa ya mpya ya mkataba wa malipo ya pauni na 200,000 kwa wiki na klabu yake ya Liverpool. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, anakaribia kusaini mkataba mpya licha ya Manchester United kumtaka Mserbia huyo pamoja na vilabu vya Paris St-Germain na Juventus. (Daily Mail)

Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Uholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28

Meneja wa zamani wa Leicester Mfaransa Claude Puel ndiye mtu anayetazamiwa kuchukua nafasi ya meneja katika klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon.(L'Equipe)

Marcos Rojo, 29, atalazimisha kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari , baada ya mlinzi huyo wa Argentina kushindwa kuondoka Old Trafford katika dirisha la usajili lililoisha hivi karibuni. (Birmingham Live)

Kelechi Nwakali, 21, ambaye alihamia katika klabu ya daraja la pili ya Uhispania, Huesca kutoka Arsenal msimu huu , anataka kurudi katika uwanja wa Emirates siku zijazo . (Score Nigeria via Football.London)

Beki wa England Danny Rose, 29, anataka kuendela kupigania nafasi yake katika timu ya Tottenham Hotspur licha ya kwamba klabu nyingine zimeonyesha kumtaka na kuwasili kwa Ryan Sessegnon, mweny umri wa miaka 19, kutoka Fulham. (Mirror)

Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 29, atalazimika kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari

Real Madrid watagrejelea tena haja yao ya kumsaka kiungo wa kati wa Ajax - Donny van de Beek,mwenye umri wa miaka 22, katika kipindi cha msimu kuhama kwa wachezaji cha majira ya kiangazi cha mwaka 2020 . (Daily Mail)

Leeds wanakaribia kabisa kuongeza zaidi mkataba wa miaka mitano na kiungo wa kati wa Kalvin Phillps mwenye umri wa miaka 23 ,baada ya Aston Villa na Burnle kuonyesha nia za kumnunua mchezaji huyo katika kipindi cha mechi za kipindi cha kabla ya kuaza kwa msimu wa michezo . (Telegraph)

Mchezaji wa safu ya nyuma wa Italy ukipenda full-back -Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, anasema hajutii kitendo chake cha kuhamia Manchester United,paada ya kujiunga na Parma kuhfuatia misimu minne akiwa katika Old Trafford. (Football Italia)

Mlinda lango wa Stalwart Germany na Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, hana mipango ya kustaafu . (Mirror)

Waziri mkuu wa Albania Edvin Rama amefichua kuwa mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron aliomba msamaha wa dhati baada ya kupigwa kwa wimbo wa taifa ambao sio wa Albania kwa ajili ya timu ya nchi yake katika mchezo wa timu zilizofuzu kwa ajili ya kombe la Euro 2020 wakati wapocheza na timu ya Ufaransa mjini Paris. (Goal.com)


Mwanza. Wakati ikihitimisha tukio la Wiki ya Mwananchi kwa Kanda ya Ziwa jijini Mwanzai, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameifananisha klabu hiyo na Barcelona ya Hispania, akisisitiza kuwa  watatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu wamejipanga vizuri.

Zahera alisema hata timu za Ulaya hufungwa, lakini mwisho hutangaza ubingwa, hivyo Yanga haitakata tamaa katika mashindano mbalimbali inayoshiriki ikiwamo mchezo wao na Zesco ya Zambia utakaopigwa wiki ijayo ambao utatoa mwelekeo kuelekea hatua ya makundi ya ligi hiyo.
Alisema amesikiliza kwa umakini vilio vya mashabiki wa timu hiyo wanaotaka itinge hatua ya makundi, lakini ahadi yake kwao ni moja tu, watatinga.

Zahera alisema zipo timu barani Ulaya huanza vibaya michezo zinayoshiriki kwa kufungwa, lakini kadri inavyoendelea hujikuta zinamaliza na ubingwa mikononi na ndivyo itakavyokuwa kwao. Yanga ilifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Agosti 28. 

“Mechi moja tu ndio itupotezee ndoto za ubingwa? Barcelona waliwahi kufungwa mechi ya awali kabisa lakini walitangaza ubingwa, kwa hiyo hata sisi Yanga itakuwa hivyo,” alitamba Zahera.
Kocha huyo mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa Jangwani, alisema malengo ya timu ni kufuzu kwanza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku hesabu zingine zikiwa za kubeba taji la Ligi Kuu Bara.

Aliwasifia nyota wake akisema kwa sasa wanampa furaha kutokana na jinsi wanavyomwelewa mazoezini na kwamba, mchezo wa Jumamosi dhidi ya Zesco ni lazima wafanye kweli.
“Nashukuru vijana wanaenda vizuri, wananielewa ninachowaelekeza hata ambao hawapo kambini, lakini huko walipo kwenye timu ya Taifa wanafanya mazoezi, kwa hiyo sioni tatizo,” alisema.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla aliwaahidi mashabiki wa timu hiyo Kanda ya Ziwa kuwa, iwapo itatinga makundi ya Klabu Bingwa Afrika watahamishia michezo hiyo katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa.

Dk Msolla alisema hatua hiyo inatokana na mazingira mazuri ya Jiji la Mwanza ikizingatiwa kwamba mbali na Uwanja wa Taifa, dimba lingine ambalo walijaza kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kulitumia ni lile la CCM Kirumba na kwamba wanaamini wakiwa jijini hapa kila kitu kitakwenda vizuri.

Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Mwanza, Saleh Akida alisema wamejipanga kuhakikisha timu hiyo inapata mafanikio inapokuwa mkoani humo.


Tokeo la picha la juma kaseja

JUMA Kaseja mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa kinachomfanya awe bora siku zote ni kipaji alichopewa na Mungu.

Jana Kaseja aliibuka shujaa baada ya kuokoa penalti moja kwenye mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022 dhidi ya Burundi uliochezwa Uwanja wa Taifa.



Stars ilipenya hatua ya makundi kwa ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilka kwa timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

"Nimecheza ligi kwa muda wa zaidi ya miaka 19 na hakuna mwalimu ambaye amewahi kunifundisha kudaka penalti zaidi ya kipaji nilichopewa na Mungu, sina kingine cha kusema zaidi ya kushukuru sapoti na kufanya makubwa kwa ajili ya Taifa letu," amesema Kaseja.

 Mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi timu zote zilitoshana kwa kufungana bao 1-1.

ILI KUPATA HABARI MBALIMBALI ZA MICHEZO PAKUA APP YA MICHEZO FORUM KATIKA PLAYSTORE BOFYA HAPA KUPAKUA

Miamba hiyo ya Hispania, Los Blancos walikuwa na mpango wa kunasa saini ya kiungo huyo ambaye Man United walidai watakuwa tayari kumuuza kwa ada ya Pauni 150 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND. IMEFICHUKA kwamba Paul Pogba amebaki Manchester United kwa sabbu tu ya wadhamini kampuni ya Adidas.
Kiungo huyo ametajwa karibu muda wote wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kwamba anataka kuondoka Old Trafford kwenda kukipiga huko Real Madrid.
Miamba hiyo ya Hispania, Los Blancos walikuwa na mpango wa kunasa saini ya kiungo huyo ambaye Man United walidai watakuwa tayari kumuuza kwa ada ya Pauni 150 milioni.
Lakini, Pogba amebaki kuwa mchezaji wa Man United na taarifa zilizopatikana ni kwamba kampuni ya Adidas ndio sababu kubwa ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuendelea kubaki huko Old Trafford.
Kampuni hiyo ya Kijerumani ndio kwanza ipo kwenye mwaka wa tatu kati ya miaka 10 ya mkataba wao na mchezaji huyo, wenye thamani ya Pauni 31 milioni. Lakinni, pia ndio wanaotengeneza jezi za miamba hiyo ya Old Trafford kwenye dili lao lenye thamani ya Pauni 750 milioni ambalo liko hadi hadi 2024.
Kumekuwa na maelezo kwamba Adidas imehakikisha kwamba Pogba anaendelea kubaki kwenye kikosi cha Man United walau kwa mwaka mmoja zaidi. Chanzo cha ripoti kilibainisha: “Walikuwa kama wasuluhishi kati ya mchezaji, wakala wake na klabu.
“Adidas walikuwa watu muhimu katika kuziweka kawa pande zote kuondoa tofauti ambazo ziliibuka katika kipindi cha mchakato huo.”
Adidas pia ndio wanatengeneza jezi wa Real Madrid, lakini Pogba ni mmoja tu wa mastaa kibao wanaomilikiwa na kampuni hiyo, ambapo wengine baadhi ni Gareth Bale na Karim Benzema.
Mechi 3 zijazo za Man United
Sept 14 vs Leicester City - nyumbani
Sept 19 vs Astana - nyumbani
Sept 22 vs West Ham - ugenini

Barcelona wanajiandaa kusaini mkataba na mshambuliaji wa mbele Lionel Messi, 32

Barcelona wanaandaa mkataba mpya wa mshambuliaji Lionel Messi, 32, ambao utambakisha nyota huyo Camp Nou kwa miaka iliyosalia ya maisha yake ya soka. (Mundo Deportivo via Mirror)

Chelsea inaweza kulazimika kumpa mkataba wa muda mrefu beki wake wa kushoto Mbrazil Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 25, ambaye kocha Maurizo Sarri anamyemelea kumpeleka Juventus. (Express)

Manchester United na Manchester City wapo mbioni kupambana kumsajili kiungo wa wa Benfica Florentino Luis mwenye umri wa miaka 20. (Star)

Paul Pogba

Kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27, aliamua kusalia Manchester United badala ya kuhamia Real Madrid kutokana na mkataba wa pauni pauni 150 wa udhamini wa michezo . (The Sun)

Beki wa timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk, 28, ameshangazwa na maneno kuwa atapewa ofa ya mpya ya mkataba wa malipo ya pauni na 200,000 kwa wiki na klabu yake ya Liverpool. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, anakaribia kusaini mkataba mpya licha ya Manchester United kumtaka Mserbia huyo pamoja na vilabu vya Paris St-Germain na Juventus. (Daily Mail)

Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Uholanzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28

Meneja wa zamani wa Leicester Mfaransa Claude Puel ndiye mtu anayetazamiwa kuchukua nafasi ya meneja katika klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon.(L'Equipe)

Marcos Rojo, 29, atalazimisha kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari , baada ya mlinzi huyo wa Argentina kushindwa kuondoka Old Trafford katika dirisha la usajili lililoisha hivi karibuni. (Birmingham Live)

Kelechi Nwakali, 21, ambaye alihamia katika klabu ya daraja la pili ya Uhispania, Huesca kutoka Arsenal msimu huu , anataka kurudi katika uwanja wa Emirates siku zijazo . (Score Nigeria via Football.London)

Beki wa England Danny Rose, 29, anataka kuendela kupigania nafasi yake katika timu ya Tottenham Hotspur licha ya kwamba klabu nyingine zimeonyesha kumtaka na kuwasili kwa Ryan Sessegnon, mweny umri wa miaka 19, kutoka Fulham. (Mirror)

Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 29, atalazimika kuhamia Aston Villa kutoka Manchester United mwezi Januari

Real Madrid watagrejelea tena haja yao ya kumsaka kiungo wa kati wa Ajax - Donny van de Beek,mwenye umri wa miaka 22, katika kipindi cha msimu kuhama kwa wachezaji cha majira ya kiangazi cha mwaka 2020 . (Daily Mail)

Leeds wanakaribia kabisa kuongeza zaidi mkataba wa miaka mitano na kiungo wa kati wa Kalvin Phillps mwenye umri wa miaka 23 ,baada ya Aston Villa na Burnle kuonyesha nia za kumnunua mchezaji huyo katika kipindi cha mechi za kipindi cha kabla ya kuaza kwa msimu wa michezo . (Telegraph)

Mchezaji wa safu ya nyuma wa Italy ukipenda full-back -Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, anasema hajutii kitendo chake cha kuhamia Manchester United,paada ya kujiunga na Parma kuhfuatia misimu minne akiwa katika Old Trafford. (Football Italia)

Mlinda lango wa Stalwart Germany na Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, hana mipango ya kustaafu . (Mirror)

Waziri mkuu wa Albania Edvin Rama amefichua kuwa mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron aliomba msamaha wa dhati baada ya kupigwa kwa wimbo wa taifa ambao sio wa Albania kwa ajili ya timu ya nchi yake katika mchezo wa timu zilizofuzu kwa ajili ya kombe la Euro 2020 wakati wapocheza na timu ya Ufaransa mjini Paris. (Goal.com)

Uhamisho huo umemfanya Maguire ampiku Van Dijk, ambaye awali alikuwa akishikilia rekodi hiyo ya kuwa beki ghali duniani aliponaswa kwa Pauni 75 milioni miezi 20 iliyopita.

LIVERPOOL, England. LIVERPOOL inajianda kumpa ofa tamu Virgil van Dijk wakimpa mshahara wa kibosi zaidi huku ikidaiwa kwamba sababu kubwa ni Harry Maguire wa Manchester United.
Man United iliweka rekodi ya kumnasa Maguire kwa pesa ndefu na kuwa beki ghali zaidi duniani, walipomnyakua kwa Pauni 80 milioni akakipige huko Old Trafford.
Uhamisho huo umemfanya Maguire ampiku Van Dijk, ambaye awali alikuwa akishikilia rekodi hiyo ya kuwa beki ghali duniani aliponaswa kwa Pauni 75 milioni miezi 20 iliyopita. Lakini, sasa akiwa bora na cheo chake hicho amepokonywa, Liverpool wanatafuta namna nyingine ya kumfanya hadi ya Van Dijk kuendelea kuwa juu.
Wakati mkataba wake wa sasa ukiwa umebaki miaka minne na mshahara Pauni 125,000 kwa wiki, kuna dili tamu mezani, Liverpool wakitaka adumu kwenye timu yao huko Anfield kwa miaka sita zaidi na mshahara utakaokaribia Pauni 200,000 kwa wiki.
Jambo hilo litamfanya Mdachi huyo kuendelea kubaki Anfield hadi mwaka 2025. Baada ya kunaswa kwa pesa ndefu, Maguira ameripotiwa kulipwa mshahara wa Pauni 190,000 kwa wiki, hivyo Liverpool nao wanamtaka beki wao alipwe mshahara kama huo.
Van Dijk alikuwa mchezaji muhimu wakati Liverpool iliponyakua taji lao la sita la Ulaya na mwaka huu anapewa nafasi kubwa ya kubeba tuzo ya Ballon d'Or. Beki huyo wa zamani wa Celtic na Southampton, ameshabeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na ameingia kwenye tatu bora ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Fifa sambamba na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.


Uongozi mpya wa Klabu ya Yanga ulioingia madarakani chini ya mwenyekiti wake, Mshindo Msolla na makamu wake, Frederick Mwakaleba umefanikiwa kukusanya shilingi 3,935,000,000 ndani ya miezi minne tangu walipoingia madarakani.

Viongozi hao waliingia madarakani Mei 5, mwaka huu baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.

Msolla na Mwakalebela kabla ya kuingia madarakani katika kampeni zao waliahidi kuipambania klabu hiyo kwa kuhakikisha wanaongeza vyanzo vya mapato kupitia udhamini mbalimbali wa makampuni.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Championi Ijumaa, Yanga hadi hivi sasa ina udhamini wa makampuni saba ambayo yote yamemwaga mamilioni na mabilioni ya fedha.

Makampuni na viwango vya fedha walizomwaga ni Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa iliyoweka udhamini wa Sh bilioni 1.94 ambao umeboreshwa hivi karibuni baada ya viongozi hao kuingia madarakani wakati awali walikuwa na mkataba wa Sh Mil 970.

Kampuni nyingine ni GSM walioshinda tenda ya uuzaji wa jezi za Yanga iliyotoa Sh bilioni 1.3, pia kampuni hiyo imeongeza fedha kwa kutoa Sh milioni 150 ya udhamini kupitia magodoro yao ya GSM.

Wadhamini wengine ni Taifa Gas chini ya mfanyabiashara, Rostam Aziz ambapo wamekubali kutoa Sh 300m kwa ajili ya udhamini, ambapo tayari Yanga wameshaanza kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini huyo begani.

Dili lingine ni kuwa Azam TV wanaonyesha kipindi cha Yanga TV ambapo kupitia kipindi hicho Yanga wananufaika kwa kupata Sh milioni 100, udhamini mwingine ni Afya Maji wenye thamani ya Sh milioni 100 huku Vodacom wanaodhamini Ligi Kuu Bara wakiinufaisha klabu hiyo kwa Sh milioni 45.

Jumla ya udhamini wote ni Sh bilioni 3.93 ambazo viongozi hao wapya wamezipata ndani ya kipindi kifupi cha miezi minne.

Akizungumzia hilo juzi kwenye kikao cha viongozi wa matawi wa Yanga kilichofanyika kwenye Makao Mkuu ya Klabu ya Yanga, Msolla alisema: “Mpaka hivi sasa Yanga ina mkataba na Sportpesa ambao mwaka huu watatoa Sh bilioni 1.94.

“Uongozi umefanikiwa kupata mikataba na Taifa Gas kutoka kwa Rostam ambao watatoa milioni 300, lakini pia ushirikiano na mheshimiwa Rostam bado upo, ndiye aliyetoa Sh milioni 60 kuvunja mkataba wa Kindoki na fedha za kumleta Molinga Yanga.

“Mkataba wa kwanza na GSM ni ule wa jezi ambao klabu itapata shilingi 1,300 kwa kila jezi itakayouzwa na lengo ni kuhakikisha jezi milioni moja zinauzwa ili klabu ipate Sh bilioni 1.3, pia mkataba unahusisha ukarabati wa Jengo la Yanga.

“Mkataba wa pili na GSM unahusisha magodoro ya GSM mkataba huu una thamani ya milioni 150, pia klabu ipo mbioni kuongeza mdhamini mwingine kutoka kampuni ya vinywaji atakayetoa fedha kama ilivyofanya SportPesa na kukarabati ‘pitch’ ya Uwanja wa Kaunda uwe wa kisasa kutumika katika mazoezi, ndiyo maana zoezi la kuweka kifusi linaendelea kwa kasi,” alisema Msolla.



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa itakuwa kazi ngumu kwa wapinzani wao Zesco kupenya uwanja wa Taifa kwani wamejipanga kumaliza mchezo mapema kutokana na hasira walizopewa na Simba pamoja na KMC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kutolewa kwa Simba mapema licha ya msimu uliopita kufanya vema kumewapa hasira ya kupambana ili kutinga hatua ya makundi.

"Kwa sasa tunajua kwamba Simba ameshatolewa kwenye michuano hii ya kimataifa pamoja na KMC kutolewa kwao kumetufanya tuwe na hasira ya kupambana kutafuta matokeo chanya kwenye michezo yetu.

" Kufanya kwetu vizuri kutaongeza pointi na idadi ya timu shiriki tukishindwa itakuwa pigo, mashabiki watupe sapoti nasi hatutawaangusha katika hilo kikubwa ni kuamini kwamba tunaweza," amesema Saleh.

Yanga itamenyana na Zesco, Septemba 14 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wao wa hatua ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.