Baada ya mapumziko ya wiki moja kupisha mechi za kufuzu Fainali za AFCON kikosi chetu kimerejea mazoezini kujiandaa na mechi zilizosalia za Ligi Kuu ya NBC.

Kikosi kimefanya mazoezi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena chini ya Kocha Msaidizi Seleman Matola, ambapo wachezaji waliohudhuria ni wale ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa.

Kutokana na hatua hiyo, wachezaji watakuwa wanatoka majumbani kwao na kurejea ambapo wanasubiri walioitwa timu za taifa warejee ili waingie kambini pamoja moja kwa moja.

Baada ya majukumu ya timu za taifa kumalizika wachezaji walioitwa watarudi kujiunga na wenzao kuendelea na maandalizi.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.