Home
Unlabelled
KIUNGO WA SIMBA AREJEA
CLATOUS Chama nyota wa Simba huenda atakuwa miongoni mwa nyota watakaoonyesha makeke yao kwenye mechi za ligi baada ya kuwa fiti.
Mei 28, Chama alikuwa shuhuda kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kome la Shirikisho dhidi ya Yanga na timu yake ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji akiwa ni Feisal Saulu, huku jambo ambalo lilimuweka nje ikiwa ni majeraha.
Kwa sasa taarifa zimeeleza kuwa Chama amepona majeraha ya enka yaliyomuweka nje hivyo kwa mechi tano za ligi zilizobaki anaweza kuwa miongoni mwa watakaocheza.
Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Simba amesema kuwa nyota huyo alipewa mapumziko maalumu akipewa matibabu ambapo alichagua kwenda Zambia.
“Chama alikuwa anapewa matibabu na aliomba kuweza kupewa matibabu akiwa Zambia ambapo muda aliopewa na anaendelea vizuri.
“Tunaamini kwamba kwa mechi zetu tano ambazo zimebaki anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji ambao watakuwepo ndani ya kikosi,”.
Post a Comment